mwanakijiji
09-26-2009, 09:31 PM
Na Mwandishi Wetu (Mwananchi)
MBUNGE wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe ameitupia kombora CCM kwamba, baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, wameamua kumhujumu kwa kupeleka fedha za rushwa katika jimbo lake ili kumng'oa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, Mwakyembe alisema viongozi hao wamekuwa wakishirikiana na jopo la mafisadi kusambaza fedha hizo kwa wananchi wa Kyela.
Alisema hivi karibuni wabaya wake hao waliingiza mamilioni ya fedha katika jimbo hilo, zilizopelekwa na kiongozi Mwandamizi wa CCM Mkoa wa Mbeya, lakini alipewa taarifa na kuwataka wazee wazipokee na kuzitumia kwa vile ni fedha zao zilizoibwa na mafisadi.
"Mimi nimewashauri wananchi wazipokee fedha hizo na wazitumie kwa sababu ni mali yao iliyoporwa na mafisadi," alisema.
Mwakyembe alisema anashangaa kuona kwamba rushwa inayopelekwa katika jimbo lake na kusambazwa na mafisadi inajulikana na viongozi wa serikali na CCM, lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa mpaka sasa.
"Serikali ina vyombo vya dola inaweza kuchunguza, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wahusika," alisema.
Alisema njama za watu hao zinafanywa zikiwashirikisha pia baadhi ya viongozi wa serikali waziwazi bila ya kificho, hali ambayo inamfanya aamini kuwa wabaya wake wana baraka na wanayoyafanya.
Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema kama taarifa hizo zipo zitazungumzwa kwenye kikao cha ndani cha chama na si nje.
''Kama hilo lipo tutalizungumza kwenye kikao chetu, siwezi kumwaga mchele kwenye kuku wengi, hivyo akiwasilisha madai yake tutayashughulikia,'' alisema Chiligati.
Mbunge huyo ambaye aliongoza kamati ya bunge ya kuchunguza kashfa ya Richmond alijifariji kwamba, atashinda mapambano hayo kwa sababu wananchi wa Kyela bado wana imani naye.
Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka Kyela, zinaeleza kuwa baadhi ya watu waliozipokea fedha hizo walimtaarifu mbunge wao na wakakubaliana kuwa wagawane na nyingine wakanunulia vinywaji.
Mwakyembe ambaye amekuwa katika ugomvi mkubwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile kwa madai kuwa mkuu huyo wa mkoa anamhujumu akitaka kumng'oa katika jimbo hilo, alisema yote hayo anawaachia wananchi wa Kyela kuamua.
Hii ni mara ya kwanza kwa mbunge huyo ambaye yupo katika kundi la wabunge wanaopambana na ufisadi, kuwashutumu baadhi ya viongozi wa juu waandamizi wa CCM kuwa sasa wanashirikiana na wabaya wake kummaliza.
Akizungumzia uhusiano wake na Mwakipesile, mbunge huyo alisema walishasuluhishwa siku nyingi anashangaa kuona bado anaendelea kuzungumzia tofauti yao na akashauri kama hajaridhika ni vyema akalifikisha suala hilo katika ngazi ya CCM.
Hivi karibuni kumeibuka mgawanyiko wa wana CCM wanaopinga ufisadi na wana CCM ambao wako upande wa mafisadi , hali ambayo ina hatarisha uhai wa chama hicho.
Mgawanyiko huo ndani ya chama hicho ndio ambao ulikifanya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho mjini Dodoma kuunda kamati ya watu watatu wakiongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na Mwanasiasa Mkongwe nchini, Abdulrahman Kinana kufuatilia uhasama uliopo kati ya wana CCM na wabunge wa chama hicho.
Wakati akizungumza na wananchi kwa staili mpya ya kujibu maswali ya papo kwa hapo, Rais Jakaya Kikwete alisema CCM na serikali haijawafunga midomo wabunge wake kuikosoa serikali.