PDA

View Full Version : Ofisi ya rais



Dua
10-09-2009, 12:53 AM
Rais anapoanguka au kupoteza fahamu

Hivi kweli baada ya kuzimia ati nilisikia alirudi na kuendelea na risala au hotuba sijui ni nini? Hivi kweli Wabunge wote wanafanywa watoto wadogo na kuendekeza huu ujinga. Jakaya Kikwete ni mgonjwa na wakati wowote jambo lolote linaweza kutokea, kwa nini wabunge waliopewa dhamana wanaweka maisha ya Watanzania million 40 kwenye mashaka ya kuwa na kiongozi ambaye uwezo wake wa kuongoza hauko sawa sawa? JK hayuko fit kuongoza kwa nini anang’ang’ania madaraka na kuuza nchi kama njugu? Au kwa sababu anafahamu atatutoka hivi karibuni?

Wabunge fanyeni kazi yenu na kutuondolea hii dhihaka. Wananchi wamewapa dhamana kuona nchi haitetereki – rais mgonjwa hawezi kuwashughulikia mafisadi - muda mwingi ni wa kuangalia afya yake, hata nchi ikivamiwa atakuwa amezimia. Vifungu vipo kisheria vya kumuondoa madarakani wakati afya yake siyo nzuri na kuwa rais ni pamoja na kuwa mwenye afya nzuri wakati wote. JK afya yake zero.

geofrey mushema
10-11-2009, 05:51 PM
binafsi naamini hata hizi safari za marekani mara kwa mara ni kwa ajili ya kufanyiwa check up.kusema kweli huyu jamaa si mzima hata kidogo na sitraki kuamini kuwa anaweza kupambana na kashikashi za nguvu ya uma pindi wananchi tutakapochoka kuvumilia.

Ach-F
10-11-2009, 06:34 PM
Juzi juzi niliona Salma Kikwete akihutubia au kutoa nasaha kwenye shule moja kama sikosei Mkuranga, swali ninalopata hapa anatumia bajeti ipi? Salma hakuchaguliwa kama rais namba mbili na hayuko equipped vya kutosha kuona mbali kwenye maswala yanayohusu taifa kwa ujumla.

mwanakijiji
10-12-2009, 12:20 AM
binafsi naamini hata hizi safari za marekani mara kwa mara ni kwa ajili ya kufanyiwa check up.kusema kweli huyu jamaa si mzima hata kidogo na sitraki kuamini kuwa anaweza kupambana na kashikashi za nguvu ya uma pindi wananchi tutakapochoka kuvumilia.

Kwa kweli hali yake inashtusha na maelezo marefu ya madaktari wake yamenifanya niwe na wawasi kama atagombea tena mwakani.

Ach-F
10-17-2009, 06:05 PM
Rais Kikwete ametekwa na mafisadi kiasi kwamba hawezi kufurukuta na watanzania walio wengi hawajagundua kwamba rais wao ni mateka.

mwanakijiji
10-31-2009, 11:15 PM
Hilo wazo kwa kweli linatisha.. naombea kuwa hauko sahihi!