mwanakijiji
11-11-2009, 08:02 AM
Na Jackson Odoyo (Mwananchi)
WAFANYAKAZI wa TRL wameamua kujitwalia menejimenti ya kampuni hiyo ya huduma za usafiri wa reli baada ya kumalizika kwa muda wa notisi ya siku 60 iliyowekwa na wawekezaji toka nje ambao ni Kampuni ya Rites ya India.
Rites, ambayo inamiliki asilimia 51 ya hisa za TRL, ilitoa notisi hiyo kwa serikali Septemba 10 ikiweka masharti mengi ambayo ilitaka yatekelezwe kabla ya Novemba 10 ikitishia kusitisha mkataba wake wa miaka 25 ambao umekuwa ukilegalega kadri siku zinavyokwenda.
Uamuzi huo wa kujitwalia madaraka ulitangazwa jana na wafanyakazi hao katika mkutano wao uliofanyika kwenye karakana ya TRL, maarufu kama Kapuya Hall, jijini Dar es Salaam, ukienda sambamba na tamko la kutoitambua menejimenti ya kigeni.
Hata hivyo, wafanyakazi hao walisema watatoa taarifa zaidi baadaye juu ya namna watakavyoendesha shirika hilo ambalo pia serikali inamiliki asilimia 49.
Wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti unaolaumu watendaji wa serikali na menejimenti hiyo ya kigeni, wafanyakazi hao walisema kwa sasa wamedhibiti masuala na vyanzo vya fedha vya TRL katika vituo mbalimbali vya kampuni hiyo na kwamba kuanzia leo watadhibiti kirahisi fedha zitakazoingia.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake wakati wa kikao hicho, mmoja wa wafanyakazi hao aliyejulikana kwa jina la Bob Kuku alisema hawautambui utawala wa TRL kuanzia jana na kwamba, mambo yote yatakayofanyika katika shirika hilo sasa yatakuwa chini ya wazawa.
“Leo hii (jana) ni siku ya furaha kwetu kwa sababu tumeanza safari mpya bila utawala wa Wahindi. Hawa jamaa wametuburuza kwa kipindi kirefu huku serikali ikishindwa kuwadhibiti.
Walitoa notisi ya siku 60 kuanzia Septemba 10 mwaka huu na leo ndiyo siku ya mwisho,” alisema Bob Kuku.
Kuku aliongeza kusema: “Ingawa serikali imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu notisi hiyo, sisi wafanyakazi wa TRL tumepitisha azimio letu kwamba hatuwataki Wahindi na hatuwatambui.”
Alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakishauri serikali kuvunja mkataba na wawekezaji hao kwa kuwa wameshindwa kuendesha TRL, lakini imekuwa inawaogopa na kuhisi kuwa pengine ukimya wa serikali baada ya notisi hiyo ulitokana na kufikiria namna ya kuwaomba ili wasitishe mpango wao wa kuondoka.
“Waziri wa Miundombinu Dk Shukuru Kawambwa alikuja hapa mwezi wa nane mwaka huu ikiwa ni siku chache baada ya Wahindi kutangaza kusimamisha mabehewa yao pamoja na injini za treni, Kawambwa akasema hayatasimamishwa, lakini baadaye yakasimamishwa,” alisema mfanyakazi huyo.
“Baada ya mabehewa hayo kusimamishwa Waziri Kawambwa amekaa kimya; hakuja tena kutueleza chochote kwa sababu ameona aibu. Nina uhakika kwamba Kawambwa hawezi kufika tena kwetu kueleza chochote kuhusu TRL.”
Serikali imekuwa ikieleza kuwa inasita kuvunja mkataba huo kwa kuhofia kuingia gharama kubwa za fidia, lakini wafanyakazi hao walisema hakuna haja ya kuogopa kwa sababu wawekezaji hao hawana cha kujivunia na wanaishi kwa jasho la wafanyakazi.
Buku alisema sasa ni siku 60 tangu wawekezaji hao waliposimamisha mabehewa na injini zao za kukodi, lakini wafanyakazi wamefanikiwa kuendelea kutoa huduma kwa kutengeneza injini na mabehewa ya zamani.
“Hawa jamaa ni wahujumu uchumi kwa sababu, mwanzo walipofika hapa walitelekeza mabehewa yetu pamoja na injini wakaleta zao, baadaye wakasimamisha zao zisifanye kazi ili Watanzania wateseke na TRL ife. Walipoona tumefufua injini zetu na mabahewa yakaanza kufanya kazi, wakaamua kuandika notisi ya siku 60 ya kuvunja mkataba,” aliongeza Kuku.
Mkurugenzi wa TRL Hundi Chaudhary alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema: “Kwa leo mimi sina cha kusema kwa sababu, serikali ilipewa notisi ya siku 60 ambazo zimekamika leo, hivyo siwezi kusema chochote.
Naomba uniache tu niendelee na kazi zangu nyingine.”
Moja ya masharti yaliyoainishwa kwenye notisi ya wawekezaji hao ni pamoja na kuitaka serikali isiingilie masuala ya fedha ya TRL na pia kuitaka ilipe madeni yote, yakiwemo ya ukodishwaji wa mabehewa na injini.
Kiasi cha fedha kinachodaiwa ni dola 115 milioni za Kimarekani pamoja na mtaji wa kati ya dola 226 na 300 milioni za Kimarekani ambazo zilipaswa kutolewa wakati wa kuanza mkataba huo.
Notisi hiyo pia iliitaka serikali kuchukua hatua za haraka za kuisaidia TRL kuongeza nguvu katika kazi na kufanya mabadiliko ya hali ya kufanya kazi kwa wafanyakazi wa TRL na pia kuongeza injini za treni katika bandari ya Ziwa Victoria na kuboresha miundombinu na vitendea kazi.
Maoni:
Yawezekana huko tunakokwenda wananchi wataanza kujitwalia madaraka wao wenyewe pale wanapoona viongozi wao ni legelege?