PDA

View Full Version : Umoja wa mataifa uiombe radhi Tanzania?



mwanakijiji
11-30-2009, 03:43 PM
Habari Leo

TANZANIA imeutaka Umoja wa Mataifa (UN) kuiomba radhi kutokana na taarifa iliyotolewa na Kikundi cha Wataalamu na Wachunguzi kutoka Umoja huo kuwa inatoa na kusambaza silaha kwa kikundi cha waasi cha FDLR kinachopigana dhidi ya raia na Rwanda, Mashariki mwa Kongo.

Kikundi hicho cha wataalamu watano kinachohusishwa na UN, kilikwenda kutathmini hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na katika ripoti yake, kilidai kwamba Tanzania inasambaza silaha na kwamba viongozi wanaelewa kinachoendelea.

Kwa mujibu wa Jarida la Africa Confidential ambalo huchapishwa London, Uingereza, kikundi hicho cha wataalamu cha UN kinaundwa na watu watano kutoka Ubelgiji, Guinea, Marekani, Italia na Uingereza.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Port of Spain, Trinidad na Tobago, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema Tanzania imeshtushwa na kushangazwa na taarifa hiyo isiyo na ukweli.

Aliutaka Umoja wa Mataifa kuilaani, kuitupilia mbali taarifa hii na kuomba radhi.

?Taarifa hii haina ukweli wowote na ni ya kitapeli. Ni uongo uliotengenezwa kulipaka matope jina zuri la Tanzania na Serikali yetu,? alisema Membe.

Alisema, ?Tanzania wala vyombo vya usalama havijatoa wala kusaidia vikundi hivyo.

Tanzania inachofanya, ni kusaidia harakati za amani na usalama Mashariki mwa Kongo kwa kumteua Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuungana na viongozi wengine kutafuta amani na usuluhishi nchini humo na si vinginevyo?, alisisitiza Membe.

Membe alisema Tanzania imekwishatumia dola za Marekani 500,000 kugharimia mchakato wa amani na usuluhishi Mashariki mwa Kongo chini ya Mkapa.

Aidha, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutafuta amani katika Ukanda wa Maziwa Makuu kwa miaka 15 na kwamba tangu mwaka 1959 hadi sasa imekuwa kimbilio la wakimbizi wanaokimbia vita na mauaji kutoka nchi za ukanda wa Maziwa Makuu.

Alisema itaendelea kufanya hivyo na si kuchochea vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.

?Katika kipindi chote tangu uhuru Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutetea amani Afrika, hivi tutapata nini kuingilia amani ya nchi jirani na rafiki kama Kongo na Rwanda,? alihoji Membe.

Wakati huo huo, Membe alitoa changamoto kwa UN kuieleza Tanzania zilikotoka silaha hizo na zinavyosafirishwa kwani haikuelezwa katika taarifa ya kikundi hicho.

Alisema Tanzania haina maduka ya kuuza silaha za kivita na wala hayaruhusiwi na kwamba silaha kama hizo zipo mikononi mwa vyombo vya usalama pekee.

?Nataka kumhakikishia kila mmoja kuwa hii haijatokea na wala haitatokea kamwe. Serikali haitaruhusu vyombo vyake vya usalama kufanya hivyo na hata hivyo hakuna taarifa kutoka vyombo vya usalama kwamba vimepotelewa na silaha.

?Na hii ndio sababu inayonifanya niseme taarifa ya kikundi hicho ni uongo uliotengenezwa dhidi ya Tanzania. Nauomba Umoja wa Mataifa na kila mmoja kuilaani taarifa hii,? alisisitiza Membe.

Alisema, ?Hiki ni kitendo ni cha uadui ambacho kinatufanya iwe vigumu kwetu kubakia kimya. Tunayo haki ya kutendewa kwa namna bora zaidi. Tunastahili na tunadai kuombwa radhi.

? Membe yupo katika ujumbe wa Rais mjini Port of Spain, Trinidad na Tobago kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaotarajiwa kumalizika tarehe 29 Novemba, 2009.

Fingigwe
11-30-2009, 06:56 PM
Hapa ndipo unapopata uhakika kwamba Serikali zetu zina maslahi sana katika kuhakikisha raia wake wanakuwa kizani ama kwa elimu duni au kwa kuzidiwa na umasikini wakati wote. Vinginevyo, maelezo kuhusu viwingu kama meremeta yanashindikanaje kuwekwa wazi hadharani? Hilo jina zuri la TZ litalindwaje endapo vivuli vinaruhusiwa kutanda juu ya taasisi nyeti za nchi? Waziri asipoteze muda wake kutetea aibu hii. Serikali ianze kuchukua hatua za maana kushughulikia uozo huu angalau usiendelee kujitokeza huko mbeleni ama sivyo mustakabali wa taifa utabaki kuwa mashakani siku zote. Kama kweli ni uzushi basi mzushi wa hatari kiasi hiki atafutwe kwa dhati na kushughulikiwa ipasavyo.

Ach-F
11-30-2009, 10:42 PM
Serikali badala ya kukimbilia kuombwa radhi ionyeshe uongo wa hii team ya UN sio porojo kama za mapanki ambazo hazikuleta tija yoyote. Waeleze kinagaubaga uongo wa hiyo dosier. Njia ya mwongo ni fupi waweke viambatanisho kuonyesha uongo huo ili watu wafukuzwe kazi hakuna blah blah.

mwanakijiji
12-02-2009, 08:51 AM
Hivi ni lini Umoja wa Mataifa umeiomba radhi nchi yoyote kwa kuandika ripoti yake!?