PDA

View Full Version : Butiku na wenzake waandamwa?

mwanakijiji
12-11-2009, 07:08 PM
na Moses Ng'wat na Gordon Kalulunga, Mbeya (Tanzania Daima)

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwaweka kiporo wale wote wanaoonekana kuutilia shaka uongozi wake kwa kushindwa kuchukua maamuzi mazito, Shirikisho la Umoja wa Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya limemlaani Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku na wenzake kwa kumpinga rais katika utendaji kazi wake.

Wasomi hao walisema kitendo cha Butiku na wenzake kumshutumu hadharani Rais Kikwete katika kongamano lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kutathimini maendeleo baada ya miaka kumi ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kilitokana na fikra mgando ambazo ziliambatana na chuki ya kukosa madaraka katika serikali ya awamu ya nne.

Walisema kamwe Tanzania haiwezi kuendeshwa kwa kukosoana bila nidhamu kama wanavyofanya wazee hao ambao hata wao hawakuthubutu kulazimishwa kufanya maamuzi mazito katika enzi za utawala wao.

Wasomi hao walitoa kauli hiyo jana katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo jijini hapa baada ya maandamano ya amani ya umoja huo yaliyokuwa na lengo la kumpongeza Rais Kikwete kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2005.

Akisoma risala hiyo, Katibu wa Shirikisho la Umoja wa Wana-CCM katika vyuo hivyo, Timotheo Mzava alisema shirikisho lake linawaheshimu wazee hao, lakini wamesikitishwa na kitendo cha kutamka maneno yasiyo na mashiko kwa taifa kuipinga Serikali ya Kikwete.

?Shirikisho la Wana-CCM wa vyuo vikuu Mkoa wa Mbeya kwa kutumia ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa uhuru kila mwananchi wa kutoa maoni, tunachukua fursa hii kulaani kauli zinazotolewa na wakongwe hao wa siasa ambao wanaonekana kupoteza mwelekeo na kubaki na fikra mgando zinazolenga kuwagawa Watanzania,?? alisema Mzava

Swali:
Jamani ndio wasomi wenyewe hawa au ndio wanasiasa wenyewe hawa? MM

Dua
12-24-2009, 03:48 PM

Tanzania kumezuka tabia ya ulofa, mijitu mizima na akili zao inafanya mambo ambayo hata ukiyauliza yatakwambia unajua bila hivyo hatuwezi kuishi. Sio siri hata JWTZ hivi sasa wanafanya ujambazi wa silaha kali. I mean the country is getting worse everyday. Sijui pengine sisi tulio nje turudi na kufanya mapinduzi ya kweli kwenye sekta ya biashara n.k na kuwaonyesha kwamba it can be done.