View Full Version : Kikwete kupimwa akili.. dalili ya kuzua maswali?
mwanakijiji
12-12-2009, 12:31 AM
Alinukuluwa na gazeti la Mwananchi mara baada ya kutua toka ziara yake huko Karibiani akisema kuwa:
Nilipokuwa huko nilipima afya yangu na hasa akili na mishipa ya damu na wataalamu wakaniambia nipo salama. Ninatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya - Kikwete
Unachukuliaje kauli hiyo?
Steve Dii
12-12-2009, 04:18 AM
Alinukuluwa na gazeti la Mwananchi mara baada ya kutua toka ziara yake huko Karibiani akisema kuwa:
Nilipokuwa huko nilipima afya yangu na hasa akili na mishipa ya damu na wataalamu wakaniambia nipo salama. Ninatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya - Kikwete
Unachukuliaje kauli hiyo?
Kauli hiyo kwa vile imetolewa na mtu mwenye cheo cha Urais, inaonesha zaidi hulka ya mtoa maongezi bila kupima tathmini ya maongezi yake kwa akadamnasi iliyopo. Aidha inatokana na mtu kuzoea 'status quo' ya kutosurutishwa kwa yoyote yale atamkayo, au inatokana na mtu kuongea kwa kudharau kadamnasi iliyopo; ya kwamba haina uwezo wa kuchambua na kuona makosa ndani ya kauli. Lakini pia yaweza kuwa kauli inayoonesha mapungufu ya kweli. Yaani mtu aliyeongea hayo kwa vile ni Rais anasahau kuwa, kusema tu kuwa umeenda kupimwa akili inamaana ya kwamba kuna kitu hakiko sawa ndani ya akili kilichosababisha vipimo hivyo kuchukuliwa. Muda na wakati vipimo vilipochukuliwa, mahali na nani aliyefanya vipimo hivyo ni sababu tosha za kufanya Urais wa huyo mtu uwe batili.
mwanakijiji
12-12-2009, 07:03 AM
SteveD unajua kinachonisumbua mimi ni kuwa aliambiwa kuwa yuko "salama". Sasa mtu ambaye anapimwa akili badala ya kuambiwa ni mzima "wa afya" anaambiwa yuko "salama". Sasa mimi sielewi..!!!:confused:
Ach-F
12-12-2009, 04:17 PM
Guys akili huwa inapimwa vipi? I mean seriously how do you measure akili?
janny
04-08-2010, 11:25 AM
Kupima akili kwani walidhani akili yake haiko sawa hebu nishangae mie
janny
04-08-2010, 11:29 AM
Guys akili huwa inapimwa vipi? I mean seriously how do you measure akili?
Kwani wale wagonjwa wa akili huwa wanagundulika vip kama akili yao haiko sawa Ach-F
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.