PDA

View Full Version : "Kind" Sepetu ni mjamzito! hongera au pole?



mwanakijiji
12-12-2009, 12:37 AM
Na Joseph Shaluwa (Ijumaa)
Siku chache baada ya Miss Tanzania 2006, Wema Isaack Sepetu kutangaza hadharani kwamba ana ujauzito, wadau mbalimbali wameibuka na maswali kibao na Ijumaa ndilo gazeti pekee linaloweza kukupa kila kitu kuhusu ishu nzima.

Vingi viulizo kutoka kwa wadau hao, vinamwendea Wema ambaye anang?ara pia kwenye kiwanda cha filamu nchini, wakihoji namna ambavyo amenasa ujauzito huo na jinsi anavyojitangaza.

?Ujauzito ni jambo la kheri, ni ukuaji wa hatua, kutoka u-dada kwenda u-mama, lakini kwanini ujitangaze kiivyo? Hili ni jambo la watu wawili tu,? alisema mdau mmoja.

Kigogo mmoja mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya filamu, amesema kwamba anachokiona yeye kwa Wema ni kutapatapa, kwani kabla ya kutua kwa Chalz Baba alishakuwa na msululu wa wanaume kabla.

?Inawezekana kabisa anafanya hivi kwa nia ya kumuumiza Kanumba, maana ni hivi karibuni tu ametangaza kutafuta binti wa kuzaa naye, lakini kitu kinachoniumiza kichwa, kwanini hakuzaa na wanaume wote waliotangulia hadi akaamua kuzaa na Chalz Baba?? Alihoji Kigogo huyo ambaye aliomba sana hifadhi ya jina lake.

Prodyuza maarufu wa sinema ambaye filamu zake zinatenda vyema kunako soko, ameliambia Ijumaa kwamba, Wema alifanya haraka sana kubeba mimba ya Chalz kwani wamekuwa katika uhusiano kwa kipindi kifupi sana.

?Walitakiwa kuchunguza kwanza, hawezi kumbebea mimba mapema kiasi hiki, jamaa akimbadilikia itakuwaje? Lakini simuombei mabaya ingawa ni kweli kwamba amewahi sana,? alisema mtayarishaji sinema huyo.

Si Wema wala Chalz Baba waliopatikana kuzungumzia ishu hiyo kwani muda wote simu ya Wema ilipopigwa iliita bila kupokelewa, wakati Chalz Baba hakupatikana kabisa.

Hivi karibuni Wema alitangaza kuwa mjamzito na alieleza wazi kuwa mwenye ?mzigo? huo ni Chalz Baba ambaye naye kupitia vyombo vya habari amekiri kwamba, anajisikia vizuri sana kuwa baba watoto wa Wema.

Swali:
Yaani huyu binti hawezi kuwa na uhusiano mwingine au kufanya kitu kingine isipokuwa lazima jina la Kanumba lihusishwe?

Steve Dii
12-12-2009, 04:00 AM
Mi nasema Hongera....!

Ach-F
12-12-2009, 05:08 PM
Na Joseph Shaluwa (Ijumaa)


?Ujauzito ni jambo la kheri, ni ukuaji wa hatua, kutoka u-dada kwenda u-mama, lakini kwanini ujitangaze kiivyo? Hili ni jambo la watu wawili tu,? alisema mdau mmoja.

Kigogo mmoja mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya filamu, amesema kwamba anachokiona yeye kwa Wema ni kutapatapa, kwani kabla ya kutua kwa Chalz Baba alishakuwa na msululu wa wanaume kabla.



Swali:
Yaani huyu binti hawezi kuwa na uhusiano mwingine au kufanya kitu kingine isipokuwa lazima jina la Kanumba lihusishwe?

Kutapatapa ... ....

outlier
12-22-2009, 04:33 AM
mi naona issue kwa ujumla inakuuzwa sana;
kupata ujauzito sio issue, wanawake zaidi ya laki 1 wanapata mimba kila mwaka Tanzania!
na kutangaza sio issue vilevile, mimba sio siri useme usiseme tumbo litaonekana, na kwa wahudumu wa afya utaenda!
na kupata mimba na chalz baba na sio mwanamme mwingine, ni uamuzi tu, mambo ya amefanya haraka sijui nini, huyo jamaa atakuwa alikuwa anamtamani mwenyewe nahisi!! hata akipigwa chini, watu wanapigwa chini kila siku, so??
na watu wanaomtaja Kanumba ni ukosefu wa sera tu, na habari; huu ndio udaku wenyewe haswaa!!