PDA

View Full Version : Hakuna mgombea binafsi 2010 - serikali



mwanakijiji
12-12-2009, 11:04 PM
James Magai (Mwananchi)

SERIKALI imesisitiza kuwa suala la mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ujao haliwezekani kutekelezwa kwa sasa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali(DAG), George Masaju baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kuhamasisha wanaharakati kujiandaa na suala la mgombea binafsi na kuitaka serikali ianze maandalizi.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu yaliyoandaliwa na mtandao wa mashirika yanayotoa msaada wa kisheria, Tanlap, Tendwa alisema suala la mgombea binafsi si zawadi bali ni haki ya kila raia itakayomuwezesha kushiriki katika vyombo vya maamuzi na kwamba hiyo itawapa fursa Watanzania ambao si wafuasi wa vyama vya siasa kugombea nafasi hizo.

Lakini DAG Masaju alisema jana kuwa mchakato huo hauwezi kufanyika kwa sasa kwa kuwa suala hilo bado liko mahakamani.

Masaju alisema serikali iliamua kukata rufaa Mahakama ya Rufaa, baada ya Mahakama Kuu kuridhia kuwepo mgombea binafsi.

"Kuna watu walijitokeza wakadai kuwepo kwa mfumo huo na Mahakama Kuu ikaridhia, lakini sisi tulikataa rufaa kwa sababu tunazo sababu za msingi na suala hilo bado liko mahakamani. Hivyo mchakato huo hauwezi kufanyika kwa sasa kabla ya mahakama kutoa uamuzi," alisema Masaju.

Akizungumza na kamati ya ufundi katika mkutano uliowahusisha wakuu wa waendesha mashtaka wa kanda, wanaojadili utekelezaji wa mpango wa utenganishaji wa shughuli za upelelezi na za uendeshaji mashtaka, Masaju aliwataka viongozi hao wa kanda kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa haki kwa wakati na kuzuia uhalifu katika maeneo yao.

Aliwataka kuwa waadilifu katika kazi zao na kuepukana na tuhuma, ili kutoa taswira nzuri ya idara hiyo nyeti kwa jamii.

Ach-F
12-12-2009, 11:36 PM
CCM wanaogopa akina siye tukigombea tutawapiga mweleka.