PDA

View Full Version : Barabara ni Sera za vyama au haki yetu?

barabara
12-16-2009, 07:54 PM
Ndugu Wadau,

Nabisha hodi kwa kuhoji maoni yenu kuhusu uendelezaji wa miundombinu yetu. Tunahitaji Barabara zijengwe nchi nzima kwa ajili ya maendeleo yetu bila kujali kama vyama vya siasa vinaweka swala hili kwenye sera zao au la. Tujiulize, hivi kama 2010 kikashinda chama ambacho hakikuweka Barabara kwenye sera zake ina maana wakimalizia ujenzi wa barabara walizozikuta na wakianza kujenga barabara mpya watakuwa wanaiba sera za Chama tawala cha sasa?
Tukubaliane mambo ya msingi kitaifa ili barabara zijengwe kwa kuzingatia umuhimu sio mpaka Waziri fulani atoke eneo lako ndio mjengewe barabara. Pia kama mkichagua chama cha upinzani basi muadhibiwe kwa kunyimwa Barabara!

Sielewi kama mnaonaje ndugu zangu, maana hizi priority zinazojitokeza ki-zima moto ndio ufisadi kama wa Richmond unatokea!:confused::confused:

Ach-F
12-16-2009, 08:43 PM

Baada ya Tanzania kuingia kwenye vyama vingi serikali ilipoteza mwelekeo na kuona mwanya wa kutokutenganisha mambo yanayohusu vyama na serikali. Hapa bado WTZ wengi wako ndotoni, tungoje waamke au tuwaamshe kwa nguvu ili waondoe ukoma wa Chama tawala. Njia kuu za uchumi ni lazima ziwe chini na mikononi mwa serikali na serikali lazima ione umuhimu wake katika kuinua kiwango au kuweka standards za hali ya juu kwenye utekelezaji wake. Hivi sasa ni ndoto tu inayoendelezwa na Majangili.

barabara
12-19-2009, 11:29 AM
Njia kuu za uchumi ni lazima ziwe chini na mikononi mwa serikali na serikali lazima ione umuhimu wake katika kuinua kiwango au kuweka standards za hali ya juu kwenye utekelezaji wake. Hivi sasa ni ndoto tu inayoendelezwa na Majangili.

Sawa kabisa ndugu yangu. Hivi ni haki serikali kutenga fedha za kujenga Barabara ya Bagamoyo - Msata ambapo tayari kunafikika kwa lami kupitia Chalinze wakati wananchi wa KIGOMA, KASULU, KIBONDO wanaendelea kupigwa danadana? Wananchi wa TABORA wanaonaje barabara yao kuelekea NZEGA? Au bado wanafurahia kutegemea Treni ambayo haipo?

Hivi wabunge walivyolalamika kuhusu kujengwa Barabara ya MKATA - HANDENI - DUMILA wakati wananchi wengine hata Regional HQ hazina Lami walijibiwaje?

Unaweza kuelewa Barabara mpya zilizotajwa juu zimepita katika majimbo wanayotoka watu gani maarufu?

TUAMKE JAMANI.

mwanakijiji
12-19-2009, 09:47 PM
Barabara... unachosema Nyerere alikielezea wakati fulani akitolea mfano nchi kama Marekani na kuelezea kuwa tofauti za vyama vya republican na democrat siyo katika mambo ya msingi; Karibu wote wanakubaliana kuhusu ulinzi, afya, n.k tofauti iko katika details zake na jinsi ya kufikia malengo hayo.

Kwa Tanzania bahati mbaya sana tunahusisha mambo ya msingi na chama cha siasa kana kwamba chama cha siasa kikiondolewa madarakani basi mambo fulani ya msingi hayatofanyika. Ni muhimu kama taifa tuweke mambo yetu ya msingi kwanza ambayo tayari tunajua ni changamoto kwa taifa. Hayo ni elimu, miundombinu, afya, nishati n.k