mwanakijiji
12-27-2009, 06:11 AM
Baada ya tuhuma za wizi mkubwa katika historia ya Taifa kufanyika katika taasisi nyeti ya Benki Kuu, taasisi hiyo haijatulia kujisafisha na uongozi wa kisiasa umeshindwa kuisafisha na badala yake kama ilivyokuwa kwenye TANESCO, ATCL, TRL, na taasisi nyingine zinazopokea ruzuku toka serikalini Benki Kuu imeanza kujipongeza kwa kutumia fedha kwa kadiri inavyotaka na wakati mwingine kuhusishwa na ubadhirifu mpya.
Mpango wa kutoa mikopo ya mamilioni kwa watumishi wake na matumizi ya karibu shilingi bilioni moja na nusu kujenga upya jumba la Gavana vimeendelea kuonesha kuwa taasisi hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi iko mbali sana na usafi na kwa kadiri muda unavyokwenda kuna uwezekano wa kashfa nyingine kubwa zaidi.
Kutokana na tuhuma hizi mpya taarifa nyeti zinadokeza kuwa mpango wa mikopo umesitishwa kwa sasa huku uongozi wa Benki Kuku ukijitahidi kuhalalisha matumizi yake ya mabilioni ya shilingi katika miradi ambayo ikipimwa vizuri inaonekana kuwa ina utata.