View Full Version : Ni mcheza filamu yupi wa Kibongo ni mkali zaidi?
mwanakijiji
12-31-2009, 08:51 AM
Kuna watu wanajitangaza kuwa wao ndio walio bora na hujionesha hivyo. Katika kuangalia angalia filamu mbalimbali za Kibongo nimefikia hitimisho kuwa yule anayejiita "the great" sidhani kama ndiye mcheza filamu bora zaidi wa kibongo kwani wavumao baharini papa, kumbe wengine pia wapo.
Kwa upande wa wanaume ni mcheza filamu gani unafikiri yuko juu na upande wa kina dada ni nani ukimuona kwenye movie unasema hii movie itakuwa nzuri?
Binafsi kwa upande wa kina kaka kuna Juma Kilowoko
Kina dada bado nafuatilia...
Max Shimba
01-25-2010, 07:07 PM
Binafsi sijabahatika kuona sinema za Tanzania. Ingawa namuona sana Kanumba kwenye magazeti na mitandao, sijui kama kuna uhusiano wowote na ujuzi unapokuwa kwenye mtandao sana.
Hivi Serikali yetu imesha wahi kufikiria kusaidia hii biashara ya cinema na musiki ambayo imewapa ajira maelfu ya vijana?
mwanakijiji
01-25-2010, 08:15 PM
Binafsi sijabahatika kuona sinema za Tanzania. Ingawa namuona sana Kanumba kwenye magazeti na mitandao, sijui kama kuna uhusiano wowote na ujuzi unapokuwa kwenye mtandao sana.
Hivi Serikali yetu imesha wahi kufikiria kusaidia hii biashara ya cinema na musiki ambayo imewapa ajira maelfu ya vijana?
Mzee unaweza kuwapima hao hapa: HAPA (http://www.greatlakesmix.com)
janny
04-08-2010, 12:19 PM
Mcheza Filamu wa kibongo mie naona kuna watu wanapewa majina makubwa lakini wawapo kwenye fani sijaona hata mmoja akiuweka uhalisia wa picha zaidi ..kuna Binti mmoja anaitwa Davina kama sikosei pia alikuwa kaole Group anajitahidi sana kuigiza katika uhalisia ingawa sijawahi kumuona front page hata moja ...
Ila kama atapata mafunzo ya sanaa anaweza kuwa hazina kwenye ulimwengu wa movie TZ
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.