PDA

View Full Version : Wahadhiri wadai kusingiziwa na ITV!

mwanakijiji
11-06-2008, 12:11 AM
Habari Leo

Kamati ya Wahadhiri wa dini ya Kiislamu nchini, wamekanusha habari iliyotangazwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, iliyodai kuwa kuna kikundi cha dini ya Kiislamu kinachotumika kuchafua jina la mfanyabiashara maarufu na mwanasiasa nchini kwa kutumia nembo ya udini na ukabila.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Chifu Hussein Msopa, alizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, na kutoa tamko la kukitaka kituo hicho cha utangazaji kuiomba kamati hiyo radhi kwa kipindi kisichopungua siku saba kuanzia jana.

?Sisi tulikuwa kwenye mkutano wetu siku hiyo, hatukualika vyombo vya habari tulikuwa tukijadili masuala matatu; OIC, Kadhi na ukabila,? alisema Msopa, na kuongeza kuwa katika ajenda hizo, walilazimika kuachana na ajenda mbili ambazo ni OIC na Kadhi kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wananchi kuiachia serikali masuala hayo.

Alisema kitu cha kushangaza ni pale televisheni hiyo ilipofuatilia kwa siri mkutano huo bila kualikwa, na kurusha mjadala na mawazo ya baadhi ya wajumbe badala ya kusubiri nini kiliamriwa au baada ya kikao, kitu kilichowatia shaka juu ya usalama wao.

Aidha, Mwenyekiti huyo alisema taarifa hiyo ilipotosha umma na kuleta uzushi na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo wanaoitakia mema dini hiyo, baada ya kueleza kuwa kikundi hicho kinachotumika kumchafua mfanyabiashara huyo, kinafadhiliwa na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Manji.

?Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba? tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho,? alisema Msopa.

Alisema kamwe Waislamu hawataacha kujadili suala la ukabila ambalo linazidi kuota mabawa nchini siku hadi siku, na kufanya baadhi ya sekta na idara za serikali kuendeshwa kikabila na bila ufanisi, sababu zinazopelekea migomo, maandamano na hata uzalishaji na huduma mbovu.

Juhudi za kumtafuta msemaji wa ITV ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile, hazikuzaa matunda, baada ya Katibu Muhtasi wake, kueleza kuwa anahudhuria mkutano, na kwamba hatazungumza na mtu ye yote. Kwa mujibu wa maelezo ya Msopa, taarifa hiyo ilitangazwa na kituo hicho Novemba 3, mwaka huu na kurudiwa siku iliyofuata, pamoja na kuonyesha picha za wahadhiri hao wakihudhuria kikao hicho.

My Take:
Ina maana tusubiri zipite siku saba ili tujue ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya ITV.

mchukia fisadi
11-09-2008, 02:18 PM
Habari Leo

Kamati ya Wahadhiri wa dini ya Kiislamu nchini, wamekanusha habari iliyotangazwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, iliyodai kuwa kuna kikundi cha dini ya Kiislamu kinachotumika kuchafua jina la mfanyabiashara maarufu na mwanasiasa nchini kwa kutumia nembo ya udini na ukabila.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Chifu Hussein Msopa, alizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, na kutoa tamko la kukitaka kituo hicho cha utangazaji kuiomba kamati hiyo radhi kwa kipindi kisichopungua siku saba kuanzia jana.

“Sisi tulikuwa kwenye mkutano wetu siku hiyo, hatukualika vyombo vya habari tulikuwa tukijadili masuala matatu; OIC, Kadhi na ukabila,” alisema Msopa, na kuongeza kuwa katika ajenda hizo, walilazimika kuachana na ajenda mbili ambazo ni OIC na Kadhi kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wananchi kuiachia serikali masuala hayo.

Alisema kitu cha kushangaza ni pale televisheni hiyo ilipofuatilia kwa siri mkutano huo bila kualikwa, na kurusha mjadala na mawazo ya baadhi ya wajumbe badala ya kusubiri nini kiliamriwa au baada ya kikao, kitu kilichowatia shaka juu ya usalama wao.

Aidha, Mwenyekiti huyo alisema taarifa hiyo ilipotosha umma na kuleta uzushi na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo wanaoitakia mema dini hiyo, baada ya kueleza kuwa kikundi hicho kinachotumika kumchafua mfanyabiashara huyo, kinafadhiliwa na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Manji.

“Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba… tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho,” alisema Msopa.

Alisema kamwe Waislamu hawataacha kujadili suala la ukabila ambalo linazidi kuota mabawa nchini siku hadi siku, na kufanya baadhi ya sekta na idara za serikali kuendeshwa kikabila na bila ufanisi, sababu zinazopelekea migomo, maandamano na hata uzalishaji na huduma mbovu.

Juhudi za kumtafuta msemaji wa ITV ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile, hazikuzaa matunda, baada ya Katibu Muhtasi wake, kueleza kuwa anahudhuria mkutano, na kwamba hatazungumza na mtu ye yote. Kwa mujibu wa maelezo ya Msopa, taarifa hiyo ilitangazwa na kituo hicho Novemba 3, mwaka huu na kurudiwa siku iliyofuata, pamoja na kuonyesha picha za wahadhiri hao wakihudhuria kikao hicho.

My Take:
Ina maana tusubiri zipite siku saba ili tujue ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya ITV.

Kama kawaida watu hawaachi kukanusha hata ukweli.
Kwa taarifa tu Msopa ajue vyombo vya habari vina haki ya kumfuatilia mtu hata kwa njia za kijasusi wakati yeye hapendi. Wakija na ukweli wa kila kitu asilalamike.
Na asijidanganye kwamba watu tutaacha kuangalia taarifa ya habari ya ITV maana ni kituo hiki tu kinatoa taarifa iliyo na utafiti wa kina.
Kama yeye na waislamu wenzie walio na nia mbaya na wakristo hawataki kuangalia sisi tusio na dini tutaangalia. Asitie shaka.

Kepa
11-12-2008, 08:08 PM
Enzi zetu magazeti yakiandika yameandika, radio na vyombo vingine vyote sheria msumeno. Siku hizi ukisoma au kusikia habari kwenye viletahabari inabidi usubiri kama week hivi ndio uweze uamini au ujue habari hiyo ni ya ukweli ama ni madudu tu. Naona kila mtu sasa awe chombo chake cha habari ni yeye mwenyewe.... Patatosha kweli? Tushike la yupi?

mwanakijiji
11-12-2008, 09:59 PM
Hivi hizo siku saba bado hazijapita tu?

Kepa
11-19-2008, 02:44 PM
Hivi hizo siku saba bado hazijapita tu?

Sasa saba zishapita!!! naona kimya meaning .. HABARI NDIO HIYO!!!

Mchungaji Ladslaus
11-24-2008, 10:06 PM
Sasa saba zishapita!!! naona kimya meaning .. HABARI NDIO HIYO!!!

Inawezekana madai ya ITV ni ya kweli, hivyo hawaoni la kushtakia
Au ndio wanajipanga ili 'kummaliza Mengi'.

mwanakijiji
11-24-2008, 10:53 PM
Nadhani hili ndio limetoka hiyo.

Kepa
11-25-2008, 01:23 AM
Ikirudi ni story nyingineeee......!!!!!

magoma
11-26-2008, 06:39 PM
YALIKUWA ya kweli ndo maana kimya, au ndo albadri inasomwa, mi naogopa