PDA

View Full Version : Wanafunzi S/Msingi walazimishwe kuimba wimbo wa taifa?



mwanakijiji
01-12-2010, 06:51 PM
Wazungu waliozuia Wimbo wa Taifa kutimuliwa
Na Richard Makore (Nipashe)

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza

Serikali imesema itawafukuza nchini wazungu wa madhehebu ya Mashahidi wa Yehova kwa kujihusisha na vitendo vya kuwashawishi wazazi katika kijiji cha Nkala, Wilaya Mbozi mkoani Mbeya na kuwazuia wanafunzi 300 kuimba wimbo wa taifa shuleni.

Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa jana jijini Dar es Salaam siku chache baada ya kuripotiwa kuwa waumini wa madhehebu ya Mashahidi wa Yehova wamewazuia watoto kuimba Wimbo wa Taifa wakati wakiwa shuleni.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, alisema jana kuwa kitendo cha wanafunzi kukataa kuimba Wimbo wa Taifa ni sawa na uhaini.

Alisema Serikali itawafukuza nchini wazungu hao ikipata ushahidi kuwa ndiyo wanaoshawishi wazazi kuwazuia watoto wao kuimba wimbo huo.

Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na viongozi wengine, kwenda kijijini hapo kufanya uchunguzi kubaini sababu za wazazi kuwakataza watoto wao kuimba wimbo huo. "Kila nchi ina Wimbo wake wa Taifa na hicho ndicho kitambulisho cha utaifa hivyo kitendo cha kuzuia wanafunzi kuimba maana yake watoto hao wanakana utaifa wao," alisema Mahiza.

Kwa mujibu wa mmoja wa waumini wa madhehebu hayo kijijini hapo, imani ya dini yao haiwaruhusu kuimba Wimbo wa Taifa wala kuisujudia Bendera kwa kuwa huyo si Mungu wao na kwamba wanaye Bwana mmoja tu ambaye ni Kristo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Nkala, Syliverster Mpemba, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tangu 2007 watoto hao walipogoma kuimba Wimbo wa Taifa na kufukuzwa shule hawajaandikishwa wanafunzi kwa ajili ya kuanza darasa la kwanza.

Alisema tangu mwaka 2007 idadi ya wanafunzi katika kijiji hicho imekuwa ikishuka kwa wastani wa watoto 90 ambao wazazi wao wanatoka madhehebu ya Mashahidi wa Yehova.