View Full Version : Tumewaharibu hawa watoto?
mwanakijiji
11-20-2008, 12:34 AM
Jumanne kundi la watoto wa shule ya msingi waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Wilaya na wao wakiwa wamekasirishwa na walimu kutolipwa na hivyo kuharibu ratiba yao ya shule. Ninapoiangaliia hii picha sikumbuki enzi zetu kama tungethubutu "kuandamana". (picha kwa hisani ya Mpoki Bukuku na Global Publishers)
wakichanja mbuga kwenda kwa Mkuu wa Wilaya
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/1.jpg
Ujumbe wao uko wazi! - wanadai "haki yao!"
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/watoto3.jpg
Wanaashiria kuwa na wao ni wazalendo wa kweli - wanapepea Bendera ya Taifa lao!
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/watoto2.jpg
Je tumewaharibu hawa watoto kwa kupandikiza fikra za kudai haki yao? Je ni mawazo gani tunayopandikiza kwa watoto kama hawa wa shule ya msingi? Kwa wanaokumbuka hii si mara ya kwanza kwa watoto wa shule ya msingi kuandamana mwaka huu. Next time chekechea nao?
Hee ama kweli wameharibiwa haswaaa. Sijui wanatokea wilaya gani.
Binafsi naona wana shida nyingi, mojawapo ambayo hawaioni kama muhimu kwao ni ukosefu wa walimu wa Sayansi kimu na walimu wa nidhamu au maadili. Na KAMA WALIMU HAO WAPO BASI HAWAJUI MAJUKUMU YAO. watoto wachafu, hawana fishikizo kwenye nguo zao/ mashati, Soksi kwao inaonekana ni anasa.
Enzi zetu tukienda maandamano ya siku kuu mbalimbali za kitaifa tulisisitizwa kuwa smart, kama huna soksi na nguo ni chafu huruhusiwi kwenda kwenye maandamano.
Watoto wetu masikini!!!!!!
mwanakijiji
11-20-2008, 07:27 AM
ila hao watoto walioshika bendera wamekaa kama viongozi wa migomo ya Chuo Kikuu huko mbeleni!
ila hao watoto walioshika bendera wamekaa kama viongozi wa migomo ya Chuo Kikuu huko mbeleni!
Mwanakijiji unadhani hawa watafika chuo kikuu kweli??? naona wameanza mapema mno...!!!
mwanakijiji
11-20-2008, 04:42 PM
Mwanakijiji unadhani hawa watafika chuo kikuu kweli??? naona wameanza mapema mno...!!!
sasa wasipofika si ndiyo itakuwa pigo kubwa sana au serikali inaweza ikaanza kuwafuatilia. Walipomkamata Mtatiro juzi polisi walimhoji kama aliwahi kushiriki katika migomo au vitu kama hivyo alipokuwa shule ya msingi!
Ach-F
11-21-2008, 12:56 AM
Jumanne kundi la watoto wa shule ya msingi waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Wilaya na wao wakiwa wamekasirishwa na walimu kutolipwa na hivyo kuharibu ratiba yao ya shule. Ninapoiangaliia hii picha sikumbuki enzi zetu kama tungethubutu "kuandamana". (picha kwa hisani ya Mpoki Bukuku na Global Publishers)
wakichanja mbuga kwenda kwa Mkuu wa Wilaya
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/1.jpg
Ujumbe wao uko wazi! - wanadai "haki yao!"
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/watoto3.jpg
Wanaashiria kuwa na wao ni wazalendo wa kweli - wanapepea Bendera ya Taifa lao!
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/watoto2.jpg
Je tumewaharibu hawa watoto kwa kupandikiza fikra za kudai haki yao? Je ni mawazo gani tunayopandikiza kwa watoto kama hawa wa shule ya msingi? Kwa wanaokumbuka hii si mara ya kwanza kwa watoto wa shule ya msingi kuandamana mwaka huu. Next time chekechea nao?
Hii inanikumbusha wakati Bokasa alipoamuru watoto wa shule kupigwa na polisi kwa kuwalazimisha kununua uniform zinazotengenezwa na mkewe. Ukiona hata watoto wanapiga kelele basi ni lazima ufahamu taifa linakwenda kubaya.
Hii sio mara ya kwanza ilitokea tena wakati wa mgogoro wa nauli za wanafunzi.
Hivi kweli tunawajali Sinclair, Dr. Dau, Barick et al kuliko hawa watoto?
mwanakijiji
11-21-2008, 05:21 AM
Yawezekana sisi tuna matatizo ya aina fulani hivi.. hadi watoto waandamane basi ni kazi.
Mpenda amani
11-22-2008, 09:36 PM
Sidhani kama wanaelewa wanachokifanya, inawezekana kabisa kuwa wanafuata mkumbo tu, wameona chuo kikuu wanagoma, walimu wanagoma, wazee wanaandamana nao wakaona ndio fashion.
Ach-F
11-22-2008, 10:34 PM
Sidhani kama wanaelewa wanachokifanya, inawezekana kabisa kuwa wanafuata mkumbo tu, wameona chuo kikuu wanagoma, walimu wanagoma, wazee wanaandamana nao wakaona ndio fashion.
Ukiona moshi ujue moto unafukuta.
magoma
11-26-2008, 07:28 PM
Kuandamana kudai haki hakumzuii mtu kwenda CHUO KIKUU, chuo kikiuu hufundishwi utii wala adabu bali unaandaliwa kuwa mtaalamu wa kitu flanu hapo baadaye na kinachokufanya ufike pale kielimu ni bidii zako za masomo huku ngazi ya chini, kwa hiyo hawa watoto hatujawharibu wako sawa na ni matunda mazuri ya viongozi wema na wanaojua HAKI ZAO NA HAKI ZA BINADAMU bila woga wowote. hiki ndo kizazi kijachokuja kisichokuwa na uoga wa amani kutoweka na kuendelea kuwa masikini milele wakati kuna watu huko juu wana templer na EPA kwa mabilioni ya shillings. sauti ya watu/watoto isikike.
duru langu
11-30-2008, 01:50 AM
Sidhani kama wanaelewa wanachokifanya, inawezekana kabisa kuwa wanafuata mkumbo tu, wameona chuo kikuu wanagoma, walimu wanagoma, wazee wanaandamana nao wakaona ndio fashion.
La hasha, wanaelewa fika kwamba wanaandamana kufikisha ujumbe wao.
Ni watoto hawa hawa ambao wanawaona dada na kaka zao au kaka wa rafiki yake
ambaye amefukuzwa chuo kikuu; ni "watoto" hawa hawa ambao wamekosa nauli ya
usafiri au matumizi kwa vile mama na baba zao hawapati mishahara yao (walimu);
Ni " watoto" hawa hawa ambao wamewona babu na bibi zao wanavyonynyasika kudai
haki zao (eac). "Watoto" hawahawa hawafundishwi kwa sababu walimu wao wanapambana na
serikali kudai haki yao.
"Watoto" hawa sasa wanaelewa kwamba haki haipatikani usipoidai na kwamba lugha wanayoielewa viongozi wetu ni ya kimapambano.
Aluta continua
Mpita Njia
11-30-2008, 11:19 AM
Sidhani kama wanaelewa wanachokifanya, inawezekana kabisa kuwa wanafuata mkumbo tu, wameona chuo kikuu wanagoma, walimu wanagoma, wazee wanaandamana nao wakaona ndio fashion.
Mkuu, nina wasiwasi sana kama watoto hawa walifuata mkumbo tu hasa ukiangalia kwa makini madai yao. Inaonekana kuwa kuna kitu ambacho hakijakaa sawa katika jamii. lakini hata kama ni kufuata mkumbo, kwa nini wafuate mkumbo huo na wasifuate mambo mengine mengi yanayotokea kwenye jamii?
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.