PDA

View Full Version : Ati wameshtushwa na kufeli!?



mwanakijiji
01-14-2010, 10:31 PM
Matokeo mabaya kidato II yaishtua serikali PDF Print E-mail
Thursday, 14 January 2010 07:55
Na Peter Masangwa

KUSHUKA kwa kiwango cha wanafunzi kufaulu kulikoonekana katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili mwaka huu kumeishtua serikali kiasi cha kuamua kukutana na wadau mbalimbali wa elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ktafuta suluhisho.

Hatua hiyo itakayowahusisha walimu wa shule za msingi, sekondari, wahadhiri wa vyuo vikuu na wadau wengine wa elimu Januari 19 mwaka huu, itakuwa na nia ya kujadili na kupata chimbuko la sababu za kudorora kwa ufaulu wa wanafunzi nchini.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza alipokuwa akitangaza matokeo ya Kidato cha Pili uliofanyika mwisho wa mwaka jana, ambapo alisema kuwa idadi ya wanafunzi waliofaulu imepungua kutoka asilimia 73.5 mwaka 2008 hadi kufikia 65.3 mwaka 2009.

Wakati hali ya ufaulu ikiwa imeshuka, Bi. Mwantumu alisema kuwa wanafunzi hao wameendelea kufanya vibaya katika masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza na kufaulu vizuri katika masomo ya Kiswahili, Uraia na Historia huku pia idadi ya vituo vilivyosajili watahiniwa kwa mtihani huo wa Novemba mwaka jana ikiwa imeongezeka kwa asilimia 6.2.

"Mwaka huu idadi ya watahiniwa waliojisajili kufanya mtihani walikuwa 394,508 lakini watahiniwa 29,547 hawakufanya mtihani bila taarifa rasmi," alisema Bi. Mahiza.

Bi. Mahiza alisema kuwa kutokana na hali hiyo serikali imeziagiza ofisi zote za ukaguzi wa shule za Wilaya na Kanda kuwasilisha taarifa ya sababu za kila mmoja wa wanafunzi ambao hawakufanya mtihani kabla ya Januari 31, mwaka huu.

Alizitaja shule tano bora za serikali zilizoongoza katika matokeo hayo kuwa ni Kibaha, Mzumbe, Ilboru, Tumaini na Msalato na tano bora za binafsi kuwa ni Feza Boys, St. Francis, Thomas Moore, Done Bosco na Feza Girls huku iliyoongoza kitaifa kuwa ni Feza boys.

Aidha alizitaja shule tano za serikali zilizoshika nafasi ya mwisho kuwa ni Somangila, Uchindule, Tegetero, Mwanagati na Mole huku shule binafsi kuwa ni Ngateu, Olmotonyi, Tabata Wazazi, Nkuhungu na Dodoma Central.

Bi. Mahiza alikiri kuwa upungufu wa miundombinu shuleni ikiwa ni pamoja na uhaba wa walimu, ukosefu wa maabara, na vifaa vya kufundishia ni mojawapo ya sababu za wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani hiyo.

"Ni kweli shule hizi za kata zilijengwa kwa kushirikiana na wazazi, hivyo mikakati iliyopo sasa ni kuhakikisha tunapata walimu wa kutosha," alisema Bi Mahiza.

Alisema kuwa baadhi ya shule za binafsi zinafanya vizuri kutokana na kuwa na uwezo wa kuajiri walimu wa kutosha wakiwemo wa kutoka nje ya nchi.

My Take:
Kabla hujasahau hebu turejee hotuba ya Kikwete ya kuaga 2009

Mkuu wa nchi alisema hivi:


Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka huu, sina budi kukiri kuwa hayakunifurahisha na kwa kweli yamenishtusha. Nimesikia maelezo mengi ya kila aina kuhusu sababu zilizochangia ufaulu wa watoto wetu kuwa wa chini kiasi hicho mwaka huu. Pamoja na yote yaliyosemwa nimewataka viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakae chini na wenzao wa TAMISEMI, Maafisa Elimu wa Wilaya na Wawakilishi wa Walimu kujadili tatizo hili kwa dhati na kutafuta ufumbuzi wake ili lisijirudie tena.

kama hilo halitoshi mitihani ya NBAA matokeo yake yalikuwa hivi:


WATAHINIWA wapatao 2,602 wamefeli mtihani wa bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu [NBAA]

Tarifa iliyotolewa na bodi na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Pius Maneno ilisema jumla ya waliofanya mtihani huo walikuwa 3,125 na kati yao watahiniwa 523 tu sawa na asilimia 16.7 walifaulu.

Kwenye NBAA waliofeli ni sawa na asilimia 84. Hii ilikuwa ni mitihani iliyofanywa mwishoni mwa 2008

Na mihitani ya mwisho ya NBAA ya 2009


WATAHINIWA 1,316 wamefeli mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) iliyofanywa Novemba mwaka huu.

Watahiniwa hao ni sawa na asilimia 42.2 ya watahiniwa wote 3,120 waliofanya mitihani hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo,Pius Maneno, amesema, watahiniwa 628 ambao ni sawa na asilimia 28.8 wamefaulu mitihani hiyo,wengine 1,156 ambao ni sawa na asilimia 31 wanatakiwa kurudia somo moja au mawili.

Well.. shule na vyuo vingi, walimu wengi, wanafunzi wengi.. matokeo chini.. Serikali ya CCM inakosea nini katika sekta ya elimu!?