PDA

View Full Version : Breaking News: Meya Kimbisa kupokea michango ya mafuriko



mwanakijiji
01-15-2010, 07:54 AM
Juhudi za taasisi ya Tanzania Professionals Network na mitandao ya JamiiForums, na Mwanakijiji na ushirika wa wananchi mbalimbali zimeanza kuzaa matunda. a

Misaada yetu ya kwanza tuliyokusanya siku hizi mbili itakabidhiwa kesho leo Ijumaa Kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar-es-Salaam Mstahiki Alhaji Adam Kimbisa majira ya saa kumi hivi (kama muda haujabadilika). Misaada hiyo ni pamoja na vitu mbalimbali vya mahitaji ya kutosheleza familia kadhaa pamoja na fedha taslimu zilizochangwa na Watanzania sehemu mbalimbali duniani.

Tunatumaini hii itakuwa ni hamasa ya kuwahakikishia watanzania wenzetu kwamba katika hili tuko makini na tunataka kuonesha kuwa tunaweza.

Taarifa ambazo bado zinaingia zinaonesha hali bado haijatulia hasa huko Kilosa kwani mto unazidi kufurika na watu wengi zaidi wanazidi kuathirika na hivyo misaada yetu inahitajika zaidi leo hii.

Kwa wale walioko Marekani unaweza kuchangia kupitia Paypal ya mtandao wa mwanakijiji.com (fedha zilizochangwa siku hizi mbili, tayari zimeshatumwa Tanzania ziunganishwe na misaada mingine). Kwenye mtandao huo unaweza kutumia kadi za Kibenki kwa njia salama kabisa (secure transaction).

Nasikia mmojawapo wa mawaziri atakuwepo kuwasilisha michango yetu hii kwa Red Cross akionesha mshikamano na umoja. Wale ambao bado wanasubiri sijaelewa wanasubiri nini hasa..

join now; be part of change, don't wait for change to happen, you'll wait unchanged!

Taarifa zaidi baadaye:


Kama uko Tanzania .. unaweza kuchangia waathirika wa mafuriko wa Tanzania:

Text "TPN" kwenda namba 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili. Na utachangia Shs 150.00 kwa siku thelathini; sawa na 4500Ths! Hii ni sawa na kuchangia dola 3.46 kwa mwezi!!



Kama uko nje ya nchi unaweza kutumia mtandao wetu hapa upande wa kulia ukurasa wa mbele au upande wa juu kwenye Forum kuna kitufye kinachosema "Donate" na unaweza kutumia kadi zozote za kibenki katika njia salama ambayo tumeshaitumia mara kadhaa katika michango mbalimbali.



the amount raised will be contributed to the Tanzanian Red Cross Society

Ach-F
01-16-2010, 05:40 PM
http://www.mwananchi.co.tz/mwanaglob/%5Craismtandaotaalumajan13.jpg


Rais wa mtandao wa wanataaluma Tanzania(TPN), Santus Mtsimbe,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana,
kuhusu TPN kwa kushirikiana na jamii Forum kukusanya Sh 10 bilioni
za kuwasaidia waathirika wa mafuriko nchini. Picha na Michael Jamson.


http://pichaz.jamiiforums.com/out.php/i1424_maafafedha.jpg

TPN, JamiiForums na Michuzi walipowasilisha michango
ya awamu ya kwanza Tanzania Red Cross Januari 15, 2010.


http://pichaz.jamiiforums.com/out.php/i1422_mafurikomsaada1.jpg

http://pichaz.jamiiforums.com/out.php/i1423_mafurikomsaada12.jpg


Meya Kimbisa pichani akipokea misaada ya awali;
Aliwashukuru wana-Mitandao na TPN kwa jitihada zao
katika janga hili na kuomba wasiache kutoa ushirikiano
pindi watakapohitajika! Misaada iliyokabidhiwa ni fedha
taslimu TZS 1,068,000.00 na vifaa vyenye thamani ya Tshs 1,400,000/=

Ach-F
02-13-2010, 11:25 PM
Flood victims get TPN donations


12th February 2010 @ 11:01

TANZANIA Professionals Network (TPN) has donated an assortment of goods worth over 4m/- to the flood victims in Morogoro and Dodoma regions respectively. The aid include 20 buckets, 20 blankets, 25 mattresses, 13 cartons of soap and 1.1m/- in cash which will be used to support communities living in the camps. The TPN Vice-President, Mr Phares Magesa, said the aid was a result of the campaign organized by TPN in collaboration with its stakeholders. The consignment was handed over to the Red Cross at its headquarters in Dar es Salaam yesterday. He said various people sent their donations to his organisation following their campaign which kicked off early January.

“This aid is a results of our initiative in collaboration with our stakeholders in order to help our fellow Tanzanians who have been affected by floods”, said the TPN vice- president. He asked Tanzanians to develop the spirit of helping one another, saying the response for helping the flood victims was not good enough. “The response actually was not adequate, we should keep on contributing since the floods have affected many people, many have lost their lives plus settlements and properties”, said Mr Magesa. Speaking on the same occasion, the Tanzania Red Cross Society Deputy Secretary General, Mr Peter Mlebusi, thanked TPN and its stakeholders for the initiative to help the people in difficulty. He said the Red Cross had targeted three areas for assistance to floods victims which include the construction of shelter, providing the victims with the health services plus non food items.

Pamoja na Mwanakijiji.com na JamiiForums kuweza kushirikiana na TPN pamoja na Michuzi Blog ni makosa makubwa ya kumfukuzisha mwanahabari wa Daily News akionekana kuandika wanaharakati hao waliojitolea kutoa misaada kwa waliokumbwa na mafuriko. Kama wewe sio mwanachama wa Chama Cha Majambazi ni adui yao hadi kufa.