Igembe Nsabo
01-16-2010, 10:46 AM
Ndugu zangu kijijini, mie naumizwa sana na hii serikali ya CCM, na huwa najiuliza sana hivi ni kwanini hatuna Mipango Shirikishi???? (Intergrated Plans)!!!, Najua kila mtu anataka huduma za msingi zifike japo mita 300 kutoka kwake na aweze kuzipata bila shida yoyote ile, lakini cha kushangaza ni kuwa TUMEKUWA NA UKARABATI NA UJENZI unaoendelea, Mfano kuna mradi wa MAJI ujulikanao kama UBORESHAJI WA HUDUMA ZA MAJI DAR ES SALAAM NA MIJI YA KIBAHA NA BAGAMOYO alimaalufu kama MRADI WA WACHINA. Ki msingi ni mradi mzuri sana na tunatengemea mengi kutokana na mradi huo ila cha kushangaza ni kuwa sasa hivi kuna mradi mwingine wa KUTANDAZA MKONGA WA TAIFA. Tatizo hapa ni kuwa hakuna mawasiliano ya karibu hapa kwani wanao chimba MIFEREJI ya Mkonga wa TAIFA hawathamini kabisa juhudi zilizofanywa na wa DAWASCO/DAWASA. Mabomba yanakatwa katwa tu na sijui hata kama DAWASA/DAWASCO wanajua hilo na wanajua kama pesa za walipa kodi zimetumika kuwalipa hawa WACHINA na kugharimia mradi mzima!!!. Siyo hayo tu ila hata Wajenzi wa Barabara kinatokea hicho hicho......, hata idara za maji nazo zinapo boresha miundombinu yake utakuta barabara nazo ziko hivyo hivyo tu, barabara imejengwa hata mwezi haujapita imebomolewa, kisa miundombinu ya maji ina wekwa!!!!!. Hizi ni pesa zetu tunalipa na tunakopeshwa tutakuja lipa, sasa kwanini tuendelee kuzichezea namna hii! na kwanini tuwaachie hawa watu wazichezee namna hii???.
SWALI HAPA ni kwanini tusiwe na Intergrated Plans (mipango shirikishi)???, Maji, Miundombinu, Mipango na Fedha wawe pamoja ili tuondokane na hii aibu ya kimasikini katika kufikilia.
SWALI HAPA ni kwanini tusiwe na Intergrated Plans (mipango shirikishi)???, Maji, Miundombinu, Mipango na Fedha wawe pamoja ili tuondokane na hii aibu ya kimasikini katika kufikilia.