PDA

View Full Version : Baba afikishwa mahakamani tuhuma ya kufanya ngono na mwanae!



mwanakijiji
01-17-2010, 04:41 AM
Baba adaiwa kufanya ngono na mtoto wake

Daniel Mjema, Rombo (mwananchi)

MFANYABIASHARA mmoja wa Rombo mkoani Kilimanjaro, Joseph Kimario (42), amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka mawili likiwemo la tuhuma za kufanya ngono na mtoto wake wa kike.

Katika kesi hiyo inayovuta hisia za wananchi wengi, mke wa mshtakiwa, Maria Joseph (32) naye ameunganishwa katika shtaka la kula njama ili kumwezesha mumewe ‘kumwingilia’ mtoto huyo.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo, Aziza Temu, huku mahakama ikiwa imefurika wananchi waliokuwa wamejawa na hasira,wakitaka kuwashambulia.

Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Richard Busimba, alidai kuwa saa 8:00 usiku wa Januari 3 mwaka huu, Kimario alifanya ngono na mtoto wake wa kike wa umri wa miaka 16.

Inspekta Busimba pia alidai kuwa katika muda huo huo wa siku ya tukio, katika Kijiji cha Kilamfue, mshtakiwa wa pili (Maria) ambaye ni mama wa kambo wa msichana huyo, alishawishi kutendeka kwa kosa hilo.

Hata hivyo washtakiwa walikana tuhuma hizo na kuiomba mahakama iwapatie dhamana kwa maelezo kuwa wao ni wafanyabiashara na kwamba kwa mujibu wa sheria, mashtaka dhidi yao yana dhamana.

Lakini kwa upande wake, mwendesha mashtaka alipinga vikali maombi hayo kwa madai kuwa kama washtakiwa wataachiwa kwa dhamana, kuna uwezekano wa kuvuruga upelelezi wa polisi kwa kutoa ushawishi, kwa mtoto wao ili asitoe ushirikiano.

Mwendesha mashtaka pia alidai kuwa kama watu hao wataachiliwa kwa dhamana, wanaweza kudhuriwa na wananchi ambao bado wana hasira nao.

Hakimu Temu anayesikiliza shauri hilo alikubali maombi hayo na kuamuru washtakiwa warejeshwe rumande hadi Januari 28 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.