PDA

View Full Version : Kweli huyu kajinyonga? (Picha kwa +18)



mwanakijiji
11-20-2008, 12:03 AM
Kuna hii habari ambayo kama kungekuwa hakuna picha ningeweza kuamini lakini hizi picha zinazua maswali mengi zaidi kuhusu habari yenyewe:

Habari yenyewe:


Na Elvan Stambuli

Mama mmoja aitwae Anjelina Renatus (27), amejinyonga kwa kutumia kanga porini na kuacha mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu akilia chini ya mti aliojinyongea.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Igagala, Mkoani Tabora.

Akisimulia mkasa huo mume wa marehemu Saidi Matoboke alisema siku hiyo mtoto wao mdogo aliyemtaja kwa jina la Hangwa alikuwa mgonjwa na waliamua kumpeleka katika Hospitali ya Misheni ya Karima ili akatibiwe.

Alisema wakati wanarudi wakiwa katikati ya pori usiku mkewe alimuomba aende akajisaidie na alipomruhusu, hakumuona tena.

Aliongeza kuwa baada ya kumsubiri kwa muda mrefu aliamua kumtafuta katika pori hilo huku akimuita jina bila mafanikio.

Aliamua kurudi nyumbani kwake katika Kitongoji cha Ugasa na asubuhi yake alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na ikaamuliwa kazi ya kumtafuta ianze mara moja.

?Mama huyo alipatikana majira ya saa 11 jioni akiwa ananing?inia juu ya mti na mtoto wake akiwa chini akilia, ni wawindaji ndiyo waliomgundua,? alisema Bw. Matoboke.

Aliendelea kusema kuwa wawindaji hao wakati wakiwinda walisikia sauti ya mtoto akilia, mara ya kwanza walidhani ni mnyama na walipofuatilia sauti ilikokuwa ikitokea walimkuta mtoto akiwa chini huku mwili wa mama yake ukining?inia ukiwa uchi wa mnyama.

Habari zinasema viongozi wa Kijiji cha Igagala walitoa taarifa polisi ambao walifika siku ya pili yake ambapo maiti ilichunguzwa na daktari kisha kuamuliwa kuzikwa.

Aidha, mtoto aliyeachwa na marehemu alichukuliwa na msamaria mwema, Bi. Mwajuma Yahya Kahungu ambaye alimpa maziwa.

Hata hivyo sababu ya kujinyonga haijaelezwa licha ya mumewe Bw. Matoboke kudai kuwa amelogwa kwani wakati akiwa kwao Shinyanga aliwahi kufanya jaribio la kutaka kujinyonga.

Katika kuonesha kuwa imani ya kishirikina imewakolea watu wa maeneo hayo, mti aliojinyongea mizizi yake imechimbuliwa kwa madai itatumika kwa dawa ambazo hazikutajwa ni za kutibu nini.

Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Jumanne Gwitagwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akafafanua kuwa miti wanayojinyongea watu hutumika kwa dawa ya magonjwa mbalimbali ambayo hakuyataja.

Picha:

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/1226990096_kajinyonga.jpg

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1226990096_mtoto.jpg

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/1226990374_kujinyongamamawamtoto.jpg

Kwa kusoma habari hiyo maswali gani unakumbana nayo ambayo yanaweza kukufanya na wewe usiamini maelezo ya Mume? Wiki hii hapa Michigan ni mwaka mmoja tangu jamaa mmoja atokee mbele ya vyombo vya habari akidai mke wake kakimbia na anamtafuta huku akitoa wito arudi. Jamaa huyo alidai kuwa walikorofishana kidogo na mke wake na alikuwa anamhisi kuwa ana cheat anapokuwa safari. Basi watu wakaanza kumtafuta huyo mama... to make the story short Jamaa amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kumuua mkewe na kumkatakata vipande vipande mbele ya watoto wao!

Kepa
11-20-2008, 01:50 AM
Mwnyekiti hapa naona inabidi uchunguzi wa kina utakapofanyika ndio ukweli utajulikana. mimi pia napata mashaka.

Mume aliacha mama aende porini kujisaidia na mtoto mgongoni, Je kulikuwa na maana gani ya mume kumsindikiza mamaaa hospitali ? halafu eti amuache polini akijisaidia hadi the next day ndo atoe taarifa kijijini? Kwa nini Imani ya kishirikiana iwe first to be pointed na mume?

Mhhh maswali mengi yanakuja hapa... nakata tamaa na siamini marehemu aliamua ghafla akajiua.

mwanakijiji
11-20-2008, 06:26 AM
Halafu ukifiria sasa mke anaenda kujisaidia, ni umbali gani huo hadi mama anaweza kuvua nguo zote, akapanda hako ka mti, akajitundika, halafu akajiachia, muda huo wote wewe mume uko wapi? Halafu mke anachelewa toka "msalani" wewe unaamua kujirudia nyumbani?

Yote Maisha
11-20-2008, 09:25 AM
Hata mimi nimepata wasiwasi kwanza hako kamti huyo mama alipandaje huko mbona
kanaonekana hakawezi kuua mtu

Degauche2008
11-20-2008, 03:01 PM
Alisema wakati wanarudi wakiwa katikati ya pori usiku mkewe alimuomba aende akajisaidie na alipomruhusu, hakumuona tena.

Aliongeza kuwa baada ya kumsubiri kwa muda mrefu aliamua kumtafuta katika pori hilo huku akimuita jina bila mafanikio.



Hapa mimi inanipa taabu kidogo, je kwanini alimruhusu kwenda kujisaidia mbali na pale walipokuwa na ilikuwa usiku? pili je kama ni kuvua nguo mbele zake ndicho mwanamke labda alichokuwa anakiongoa je hao watoto waliwapataje? Huyu jamaa aseme ukweli na kwa nini hakuutalifu uongozi wa kijiji usiku huo ili kuanza msako au majirani kama uongozi wa kijiji uko mbali. Hapana kuna mkono wa huyu jamaa.

mwanakijiji
11-20-2008, 03:40 PM
Alisema wakati wanarudi wakiwa katikati ya pori usiku mkewe alimuomba aende akajisaidie na alipomruhusu, hakumuona tena.

Aliongeza kuwa baada ya kumsubiri kwa muda mrefu aliamua kumtafuta katika pori hilo huku akimuita jina bila mafanikio.



Hapa mimi inanipa taabu kidogo, je kwanini alimruhusu kwenda kujisaidia mbali na pale walipokuwa na ilikuwa usiku? pili je kama ni kuvua nguo mbele zake ndicho mwanamke labda alichokuwa anakiongoa je hao watoto waliwapataje? Huyu jamaa aseme ukweli na kwa nini hakuutalifu uongozi wa kijiji usiku huo ili kuanza msako au majirani kama uongozi wa kijiji uko mbali. Hapana kuna mkono wa huyu jamaa.[/QUOTE]

good observation pale; kwa jinsi watu walivyorundikana hapo sidhani kama hilo pori lilikuwa ni mbali sana na makazi ya watu, na sidhani katika usiku huo huyo mama angeweza kwenda mahali kutafuta mti mzuri na kujitundika. Itabidi tumtafute huyo mkuu wa Polisi atupe habari maanake mtu anaweza akaget away with murder hivi hivi

Mpenda amani
11-22-2008, 08:52 PM
Hata bila ya kusoma hadithi yenyewe, ukitazama piacha tu huo mti ulivyokaa huyo mama nina uhakika hakukwea mwenyewe mpaka hapo juu na kufunga kanga kwenye mti na kisha shingoni alafua ajiachie? ?? no way na mtoto wa kumzaa kamuacha porini pekeyake? na kwanini avue nguo?
Na hiyo habari ya kwenda mbali huko kujisaidia??? hata kama mtu unaongozana na mkwe huendi mbali hivyo? kawaida mtu huwa anarudi nyuma hatua chache tu au kuchepuka kidogo tena ni porini wala haitaji kwenda mbali hivyo mpaka apotee. Huyo baba aulizwe vizuri tu, tatizo tu Tanzania yetu haina sheria wala hakuna watetezi wa haki za binadamu na haki za kina mama.:mad:

Kepa
11-22-2008, 11:00 PM
Huyo mume sidhani kama anatakiwa awe huru mpaka sasa. Nashangaa hata sijaona / kusoma kama ametiwa mahabu ili ajieleze vizuri. Au ndio yale ya kusema mali yangu anajilia mwenyewe msiniulize?

Eti mtu akimchinja ng'ombe wake pia mtamuuliza? hizo ndio hadithi za vijijini mara watu wanapofumaniwa na watoto wao au wajuu zao wakifanya mambo mabaya.