mwanakijiji
01-19-2010, 09:30 AM
Leon Bahati (Mwananchi)
HATIMAYE serikali imesema itauvunja mkataba wake na Shirika la Reli la India (Rates) wa kuendesha kwa ubia Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Februari, mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo alieleza hayo jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
“Tutauvunja mkataba huo kuanzia mwezi ujao (Februari),” alisema Chambo wakati wajumbe wa kamati hiyo wakimbana wakimtaka aeleze nini kinachosababisha serikali ishindwe kuuvunja mkataba huo wakati uzembe unatokana na wabia hao na siku zinavyozidi kwenda ndivyo taifa linavyozidi kupata hasara.
Chambo alikiri mbele ya kamati hiyo kwamba tatizo la TRL linatokana na uzembe wa menejimenti ambayo yote inatoka Rites.
Alieleza kinachoifanya serikali kuchukua muda mrefu ikisita kuvunja mkataba huo ni mbano wa kisheria kupitia mkataba huo ambapo serikali inaweza kujikuta inalipa mabilioni ya fedha.
Hali hiyo iliwafanya wabunge wengi watahamaki na kutaka kujua sababu zinazofanya serikali kuingia kichwa kichwa kwenye mikataba ambayo ikivunjika, hata kama ni uzembe wa mwekezaji ama mbia, Tanzania ndiyo inayoathirika.
“Inakuwaje mikataba tunayoingia, mwekezaji hata akiboronga hakuna vipengele vinavyombana yeye?” Alihoji mbunge wa Mpendae, Issa Kassim Issa (CCM).
Akimjibu, Chambo alisema: “Kweli mkataba ni mbovu, lakini tulichofanya serikali ni kuachana naye lakini tusilipe fedha nyingi.”
Aliendelea kusema kwamba tayari serikali imeupitia kwa makini mkataba huo na kuchukua vipengele ambavyo watavitumia katika kujenga hoja ya kuuvunja.
Pamoja na maelezo hayo ya Chambo kusema watatumia vipengele hivyo ili kupunguza kiwango cha fedha ambacho watapaswa kukilipa ili kuuvunja, wabunge wengi walisikitika kutokana na uzembe wa serikali kuingia mkataba huo ambao unampendelea mwekezaji hata kama makosa ni yake.
“Hivi elimu yetu Watanzania, is it fake (ni ya ubabaishaji)? Alisema Mbunge wa Nkasi, Ponsiano Nyami (CCM) na kumfanya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mohamed Rished (Pangani-CCM) kuingilia kati akimtetea Chambo asielekezewe makombora hayo.
“(Nyami) Amesema tu. Tusimbane sana kwa sababu wakati mwingine analetewa mkataba yeye ausimamie tu. Serikali na vyombo vya sheria ndio walitakiwa kuyafahamu yote hayo,” alisema Rished.
Kassim alidakia tena akishinikiza Chambo aeleze lini mkataba huo utavunjwa, ndipo akaamua kupasua jipu na kuwaambia: “Utavunjwa kuanzia mwezi ujao.”
Kamati hiyo haikumbana Chambo kwa suala hilo tu bali kulikuwepo na mlolongo wa mambo mengi miongoni ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha za kununua magari ya kifahari kwa vigogo wa serikali pamoja na ufisadi kupitia mradi wa kutengeneza mvua mwaka 2007.
Mradi huo wa kutengeneza mvua ulibuniwa na ofisi ya Waziri Mkuu, wakati huo ikiwa chini ya Edward Lowassa.
Kamati hiyo ilimbana Chambo aeleze kulikoni wizara yake kutoa Sh11.2 milioni kununua ushauri wa kutengeneza mvua wenye mashaka.
Chambo alisema kwamba mpango mzima haukuweza kufuata kanuni za sheria ya manunuzi kwa sababu ni teknolojia ambayo inatumika katika nchi mbili, China na Thailand.
Alisema China wamejiwekea kanuni ya kutotoa teknolojia hiyo kwa mataifa mengine na ndio maana wao waliwakubalia wataalamu kutoka Thailand baada ya kuruhusiwa na mfalme wa nchi hiyo.
Chambo alieleza kwamba kwa kuwa jambo hilo lilikuwa ni la ghafla ambalo lilikuwa limelenga kutatua tatizo la ukame, halikuwa limetengewa bajeti kwenye mipango ya matumizi ya serikali.
Kwa sababu hiyo, akasema ilibidi wachukue fungu hilo kwa kuminya kwenye bajeti nyingine na fedha hizo zilitumika katika kuwapeleka wataalamu hao kwenye maeneo mbalimbali ya nchi pamoja na kutembea angani kwa kutumia ndege ili kuchunguza hali ya anga la Tanzania.
Sehemu ya fedha hizo, Sh3.3 zilitumika kulipia na kuendesha mafunzo katika hoteli ya Movenpick.
“Zoezi la mvua za kutengeneza hazikuonyeshwa kwenye taarifa ya utekelezaji, hivyo wakaguzi kushindwa kutathmini thamani ya fedha zilizotumika katika kufikia lengo lililotarajiwa,” alisema Chambo.
My Take:
Hivi hii serikali walipokuwa wanatia sahihi huo mkataba walikuwa hawajui vipengele wanavyoviweka?