PDA

View Full Version : Atinga kotini kwa "shambulio la aibu"

mwanakijiji
11-21-2008, 05:05 PM
Na Saida Said, Buguruni (Dar Leo)

KIJANA David Chacha (28), mkazi wa Tabata Shule amefikishwa Mahakamani kujibu mashitaka ya shambulio la aibu kwa kumshika matiti mwanamke bila ridhaa yake.

Mshitakiwa huyo anayekabiliwa na mashitaka mengine ya shambulio mbele ya Hakimu Mussa Abdallah wa Mahakama ya Mwanzo Buguruni.

Katika mashitaka ya kwanza, imedaiwa kuwa Novemba 2, mwaka huu, saa 2 usiku, Tabata kwenye baa ya Swiss Pub, mshitakiwa David alimpiga mlalamikaji Lovenes na kumkaba shingo.

Katika mashitaka mengine imedaiwa kuwa Novemba 2, mwaka huu, mshitakiwa David alimshika matiti mlalamikaji Lovenes bila ridhaa yake.

Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na kesi itatajwa tena Desemba 11, mwaka huu.

Katika kesi nyingine,Yusuf Abdallah (24), mkazi wa Tabata Kimanga amefikishwa Mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka ya kujeruhi.

Imedaiwa mbele ya Hakimu Hamisi Masiku kuwa Novemba 8, mwaka huu, saa 5 asubuhi,Tabata Kimanga, mshitakiwa Yusuf alimjeruhi mlalamikaji Issa Bakari kwa kumkata na wembe chini ya jicho.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi itatajwa tena Novemba 24, mwaka huu.

My Take:
Hivi hizi tabia za kutomasa matiti ya mtu siyo mke wako/mpenzi wako bila ya ridhaa yake bado zipo? Hivi mtu anafikiria kwa kufanya hivyo ndiyo inakuwaje? GRRRRRRRR

Kepa
11-22-2008, 11:34 PM
Mwenyekiti umenikumbusha jambo moja linalofanana kidogo na hilo ambalo huwa linanitia aibu sana kila ninapolishuhudia kwa vijana kadha wa kadha jijini Dar.

Kwa sababu ya ugumu wa usafili na foleni, akinadada wengi wamejikuta wakibanwa sana ndani ya daladala wanapokuwa wamekosa seat wasijue ni nini kinaendelea migongoni mwao, kumbe jijana wakiume wapo kazini! vijana wanaita Kujiservia.

Tabia hii naona ikomeshwe kwa kuwafungulia mashtaka na kwa kuwaumbua wakiwa kwenye hizo harakati hata kama anayeshambuliwa hajagundua.

mwanakijiji
11-23-2008, 06:03 PM

Nakumbuka wenyewe walikuwa wanaita "kupatwa na mfadhaiko".. !

My more
11-30-2008, 12:35 AM
My Take:
Hivi hizi tabia za kutomasa matiti ya mtu siyo mke wako/mpenzi wako bila ya ridhaa yake bado zipo? Hivi mtu anafikiria kwa kufanya hivyo ndiyo inakuwaje? GRRRRRRRR Mwanakijiji

Hawa ingewezekana wafunguliwe magereza yao rasmi then, kila siku adhabu yao kabla hawajaenda kufanya kazi nyingine nzito wapewe zoezi zito la kushikwashikwa sehemu sehemu kwa dk 30, ndio wanapata heshima. Vinginevyo Wataendelea kuwashikashika wake zenu mbele yenu.

duru langu
11-30-2008, 01:20 AM
Sasa mbona mnamhukumu David mara hii? Hiyo balaa lilitokea baa na huenda huyo
dada Lovenes alipata kibano baada ya kutaka kumzidi kete David. Hilo suala la kushikwa
shikwa matiti yawezekana yakawa madai ya "kummaliza" tu David. Kwani lini masuala
ya kupakaziana yamekwisha?

My more
11-30-2008, 02:01 AM

Hivyo hivyo!!

duru langu
11-30-2008, 02:05 AM
Hivyo hivyo ndio kusema nini?

My more
12-02-2008, 01:45 AM
Hivyo hivyo ndio kusema nini?

Aliyeshikwa na Ngozi ndiye mwizi au hujui hilo?

Kepa
12-05-2008, 04:43 PM
Aliyeshikwa na Ngozi ndiye mwizi au hujui hilo?

Ndi litakuwa fundisho kwa wengine wasicheze karibu na chimo la moto/ hatari.

My more
12-08-2008, 10:46 PM
Ndi litakuwa fundisho kwa wengine wasicheze karibu na chimo la moto/ hatari.

Tena wamlete na yule mbunge aliyeenda ku wi wi barabarani, halafu alipoonwa akaanza kuwashushia watu kipigo. Aletwe haraka kwa huyu kadhi maridadi :mad::mad: