PDA

View Full Version : Bakwata kutembeza bakora kwa wanaojiachia?



mwanakijiji
02-03-2010, 08:26 PM
http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/1265179650_maureen.jpg

Na Musa Mateja
Tabia ya kutembea matiti nje inayozidi kushika kasi kama moto wa kifuu miongoni mwa mastaa ?the big name? Bongo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni ?fasheni?, sasa kuwatokea puani, Risasi Mchanganyiko limeinyaka...

Siyo siri tena kwani habari za chini ya kapeti zilizovuja zinadai kuwa, kuna mkakati kabambe unaoratibiwa na Baraza la Kiislamu nchini, BAKWATA wenye lengo la kupiga marufuku mabinti ambao ni mastaa wa dini hiyo kuacha matiti nje.
Kwa mujibu wa Shekhe mmoja ambaye hakutataka jina lake ?lipambe? ukurasa, kuacha matiti nje kwa mastaa hao kumekuwa kukitafsiriwa kuwa ni sawa na kutembea uchi.

?Kwa binti wa Kiislamu ikiwa ni pamoja na hawa mastaa wetu, kuacha matiti nje ni kuvunja maadili ya dini. Binti wa Kiislamu anatakiwa kujisitiri muda wote na kutokuacha maungo yake hadharani,? alisema.

Jamaa huyo alidai kuwa, pamoja na kuwa wanakumbushwa mara kwa mara kujiweka katika hali nadhifu, hivi sasa baraza hilo litalazimika kutembeza bakora kwa mastaa hao.

Tayari Risasi Mchanganyiko linashikilia listi ya masistaduu vinara wa kutembea matiti nje ikiwa ni pamoja na mcheza filamu ?seksi?, Aunt Ezekiel Grayson, staa mwenye heshima kwenye Bongo Flava, Kiuno bila mfupa, Rehema Chalamila ?Ray C? na ?foma? Miss Ilala, Maureen Gislary.

Wengine ni nyota wa THT, Doreen Aurelian ?Pipi?, Mcheza filamu Ndubagwe Misayo ?Thea?, Modo Fideline Iranga, Miss Tanga ?The history?, Victoria Martin na mastaa wa filamu wapenda ?promo? kama vile Miriam Jolwa ?Jini Kabula? na Jacqueline Petzel ?Jacky wa Chuz

Matigari
03-07-2010, 09:06 PM
Wakati Ukuta

mwanakijiji
03-10-2010, 07:10 AM
Kwamba yote yana mwisho Matigari?

Matigari
03-10-2010, 09:20 PM
Shukurani mwanakijiji.
Unajua huwa nakuwa na hasira kidogo na hawa viongozi wa dini wanaokimbilia siasa na adhabu kali, badala ya ku kufundisha watu kujiheshimu kwa ujumla. Yaani nidhamu iwe moyoni. Kuhusu kuwa mambo yote yana mwisho ni kweli kabisa. Akina dada ambao sasa wankaribia mika sitini, enzi zao miniskirt na minidress ilkuwa ndiyo jadi yao; walizipenda mno, walikuwa na nidhamu ya uoga, wakitoka nyumbani wanavaa khanga wakifika barbarani wanazitoa wanaendelea na matanuzi. Wakaja akina dada ambao sasa hivi wana umri wa miaka kama 48-50 hao walikuwa wanavaa maxi na midi, wenyewe wakiziita mwongozo, hivyo haya yote ni ya kupita tu. Huwa nafikiri kuwa unaishi Marekani, kama ni hivyo angalia matangazo ya nguo za spring na summer sasa hivi, ( angalia tangazo la old navy) naona hizo sun dresses zilivyo ndefu? Zinapita magotini actaually zinafika miguuni, hivyo, mini nazo zitapita, mashehe wasisitize vijana kujielimisha, kufanya kazi kwa bidii, na kujiheshimu, pia wakumbuke kuwa they will not be 20 years old for ever, they should be responsible.