mwanakijiji
11-21-2008, 05:08 PM
Na Mwandishi Wetu, jijini (Dar Leo)
WAKATI majina ya vigogo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) watakaounda sehemu ya ushahidi katika sakata zito la kesi ya wizi wa mabilioni ya pesa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), yakitajwa mahakamani jana, taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa vigogo na wazito ndani na nje ya serikali sasa wapo matumbo moto kwa hofu ya kulipukiwa na bomu hilo.
Wakili wa Serikali,Boniface Stanslaus amekaririwa na vyombo vya habari akitaja orodha ya mashahidi ambao upande wa Jamhuri unatarajia kuwaita katika kesi inayomkabili kada wa CCM, Rajab Maranda na wenzake ambao upelelezi wake umekamilika.
Alitaja majina ya mashahidi hao kuwa ni Emmanuel Boaz, Tamal Mwakilema, Elisa Masanja, Peter Nonhi, Rashid Mwanga , Samwel Mark, Athuman Mtengeti , Stella Chaula na Joseph Sheffu ambao wote ni wafanyakazi wa BoT.
Mbali ya vigogo hao pia maofisa wengine waandamizi wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi watatoa ushahidi wao.
Wakili huyo aliwataja kuwa ni Bernad Mkapa kutoka Msajili wa Kampuni (BRELA), Mwita Kaala kutoka Benki ya Biashara ya Kenya (KCB), Ronald Sifael, Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Maranda Maranda kutoka Shule ya sekondari Happy Skilful, SP Mkony kutoka Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ASP Salum Kisajo kutoka Ofisi ya Upelelezi Dar es Salaam na Jaffer Jaffer mkazi wa Kariakoo jijini.
Wakati orodha hiyo ikitajwa vigogo kadhaa wameelezewa kuingiwa wasiwasi katika hatua hiyo na kuona 'arobaini na kiyama' yao imefika.
Chanzo chetu cha kuaminika kimeeleza kuwa moja ya mambo yanawafanya vigogo hao kuhaha ni 'vinoti' na mawasiliano ya simu vinavyodaiwa kuwa huenda vilitumika kupelekeana ujumbe kwenye mchakato huo.
"Hapa hakuna atakayekubali kufa peke yake, ushahidi huu utaibua makubwa na wengi watanaswa mtegoni, ushahidi huu unaweza kuwaumbua wengi," kilisema chanzo hicho.
Kilidai kuwa inawezekana mambo hayo yalikuwa na mlolongo mrefu ulioshirikisha watu wengi hivyo suala hilo linaibua sura mpya katika sakata hilo.
"Mchezo huu haukuwa mfupi ni mrefu, watu watarajie kuona mazito mambo haya yatagusa vigogo wengi ambao nao kwa njia moja ama nyingine watajikuta pabaya. Huu unaweza kuwa mwisho mbaya wa mwaka kwao," kimesema chanzo hicho.
Kimesisitiza kuwa hatua ya kuitwa mashahidi hao hususani maofisa wa BOT ni kisu cha moto kwa vigogo wote walioshiriki kwa njia moja ama nyingine kwenye sakata hilo.