View Full Version : JamiiForums - Upgrade
Wacha
02-14-2010, 12:56 AM
Habari nilizozipata hivi punde ni kwamba Jamii Forums wanafanya upgrade ya system yao.
Hivyo wadau kutoka jamii Forums mnakaribishwa hapa kijijini mjisikie nyumbani. Taarifa zaidi zitafuata ni muda gani JF watarudi mitamboni.
Wacha
02-15-2010, 12:15 AM
Kutokana na hali isiyo ya kawaida jukwaa na ukumbi maarufu wa Jamii Forums umekumbwa na msuko suko wa mafisadi papa ambao hawaishi kujipenyeza na hawataki kuacha kula kodi ya walipa kodi bila kunawa mikono. Mtandao huo ambao umekuwa maarufu baada ya mtandao mwingine kusambaratishwa wa BCS haukuwa hewani ghafla siku ya Jumamosi na Jumapili na habari ambazo sio za ukweli ni kisingizio cha up-grades nk. Ijulikane kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi na mafisadi papa hawawezi kukubali kuondoka bila mtu.
Je, mamia na maelfu ya wanamtandao huo wana plan B? Uhuru wa kusema madudu ya Chama Cha Majambazi umekuwa unawaumiza watendaji wa kazi wa serikali kwa muda mrefu na hii inavyoelekea ni rasha rasha tu, tusubiri mvua za masika.
Wacha
02-15-2010, 02:57 AM
Mtandao wa Jamii Forums uko hewani hivi sasa.
Matigari
03-23-2010, 06:01 PM
Nashnindwa kuingia Jamii forums leo. Sijui wanatengeneza tena mitambo yao au vipi.
Leo tarehe 23 mwezi wa tatu.
Ach-F
03-23-2010, 08:12 PM
Nashnindwa kuingia Jamii forums leo. Sijui wanatengeneza tena mitambo yao au vipi.
Leo tarehe 23 mwezi wa tatu.
Ulikuwa off line kwa muda sikuweza kupata data nini kimejiri lakini hivi sasa upo hewani.
Matigari
04-01-2010, 10:05 PM
Asante sana. Japo ni zamani kidogo nisamehe kwa kutorudi na kuangalia majibu ya swali langu. Pasaka njema kwako na jamii yako.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.