PDA

View Full Version : Kachumbari ya Mayai



mwanakijiji
11-21-2008, 08:33 PM
Bi. Gladmore yeye anaelezea mojawapo ya mapishi yake:

Mahitaji


Nyanya kubwa 2
Kitunguu maji 1
Karoti kubwa 1
mayai 2
Unga wa ngano kikombe 1
Chumvi kiasi
Mafuta ya kupikia kiasi


Matayarisho:
Menya kitunguu
Osha nyanya, karoti, na kitunguu kwa maji safi

Katakati vyote kwa mkato wa miviringo isiwe minene sana wala miembamba sana, hakikikisha miviringo hiyo ipo kwenye sahani 3 tofauti ( kila kitu sahani nyake) hakikisha hakuna vipande vinavyokaa juu ya kingine.

Ponda mayai na weka ndani ya chombo kisafi
Nyunyiza chumvi kwa juu kwenye karoti , vitunguu halafu nyanya.( ili kuvifanya vitoe majimaji kidogo yatakayokusaidia kushinatisha unga wa ngano wakati wa kupika)

Haraka , weka chuma cha kukaangia motoni tia mafuta kiasi kidogo kama unapika chapati ya maji,

Mafuta yakipata moto anza na nyanya, kipande kimoja kimoja kivilingishe kwenye unga mkavu wa ngano na halafu chovya kwenye mayai na kisha moja kwa moja tia kwenye chuma cha kukaangia.

Geuza geuza visiungue kisha vikiipata rangi ya brown kwa mbali uepue.

Fanya hivyo hadi nyanya zikiisha, endelea na vitunguu (Uwe muangalifu vitunguu visiachane ile miviringo au layer yake) kisha malizia karoti.

Vipambe kwenye sahani mmoja vikiwa bado vyamoto tayari kuliwa na chips, wali, ndizi choma nk. Uwe na fresh juice kushushia.

Ukipenda waweza kutwanga pilipili mbuzi mbichi kiasi ukatia chumvi na limao ikawepo pia hapo pembeni kama monitor.

Mpenda amani
11-22-2008, 08:27 PM
Asante, nilikuwa siifahamu hii kitu, nitajaribu na mimi.

My more
11-30-2008, 02:03 AM
Asante, nilikuwa siifahamu hii kitu, nitajaribu na mimi.

Ushalijaribu eeeeh??