Ng'wana Diyu
02-26-2010, 08:39 AM
Si ajabu Chenge bado ni mwekekiti wa kamati ya maadili CCM, pia si ajabu kuwa kamati ya Mwinyi imeambiwa iwasuluhishe mafisadi na wanaopinga ufisadi. Huu ndio utawala wa sheria kwa tafsiri ya CCM na serikali yake.
Ni ajabu sana lakini ni kweli kwamba sasa hatuna serikali inayoweza kusimamia msitakabali wa taifa hili katika misingi ya sheria na bila upendeleo wowote. Kuna watu wanasota rumande kwa makosa ya uzurulaji tena kwa kuonewa, je kama si udhurulaji wale waumini wa Kakobe wanaoshinda na kukesha barabarani "wakilinda" Tanesco wasiweke nguzo kwenye kanisa lao ni nini?? Naamini kuwa nguzo zinazopitishwa na Tanesco zinawekwa katika hifadhi ya barabara ambayo si Kakobe wala mtu mwingine anaimiliki, sasa inapotokea mtu anawazuia watu wengine wasitumie kitu ambacho si mali yake na serikali inakaa kimya maana yake ni nini???????????
Na je hawa binadamu wanaoshinda na kukesha kanisani wanakula wapi?? familia zao zinalishwa na nani??
Au kuna nisiyoyajua juu ya sakata hili, wadau naomba msaada wenu