PDA

View Full Version : India ndilo suluhisho la tiba zetu?



mwanakijiji
03-04-2010, 08:42 AM
Habari Leo

MTOTO wa kike Mtanzania mwenye umri wa miaka 12 aliyeletwa hapa kutibiwa moyo, amefariki dunia kwa mshituko wa moyo akiwa katika uwanja wa ndege wa hapa.

Timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Apollo, waliwasili uwanjani hapo juzi kwa ajili ya kumhudumia mtoto huyo, lakini kwa bahati mbaya alikuwa tayari ameshakata roho. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali za Apollo, Dk. Praful Pawar, alithibitisha kuwa mtoto huyo anatoka Tanzania na alikuwa akisumbuliwa na moyo.

“Aliletwa kwenye Hospitali yetu ya Apollo na kutibiwa kwa siku 11, lakini hali yake haikuruhusu upasuaji, hivyo hakupasuliwa, alichunguzwa afya kujua kama ataweza kusafiri kwa ndege akisindikizwa na mama yake,” alisema Pawar huku akikataa kutaja jina la mtoto huyo.

Alisema mtoto huyo alikuwa na tatizo la kupumua na madaktari wa kliniki ya Apollo iliyopo kwenye uwanja huo wa ndege, walijitahidi kumwahi lakini alipatwa na mshtuko huo wa moyo na kufariki dunia kabla ya kuhudumiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha CISF uwanjani hapo, kabla mtoto huyo alipoteza fahamu mapema asubuhi siku hiyo, wakati akiwa kwenye jengo la uwanja huo akisubiri ndege.

Chanzo hicho pia kilisema siku chache zilizopita, abiria anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 55, alipatwa na ugonjwa wa moyo akiwa ndani ya ndege, hata hivyo tofauti na mtoto huyo, mwanamume huyo alipatiwa matibabu na kupona.

Kilisema pia mtoto huyo, alishapanda ndege lakini kabla haijaanza safari alishushwa kutokana na tatizo la kushindwa kupumua vizuri.

HabariLeo jana iliwasiliana na Wizara za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ya Afya na Ustawi wa Jamii, lakini wahusika walisema kwa kuwa muda wa kazi ulikuwa umepita, na maofisa wa vitengo vya nje kuondoka pengine leo wanaweza kutoa taarifa ya tukio hilo.

Pia gazeti hili liliwasiliana na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kwa mujibu wa ofisa aliyepokea, ubalozi ulikuwa umefungwa na kuitaka HabariLeo kupiga simu leo asubuhi ili kupata undani wa kisa hicho.

My Take:
Hivi kweli India ndiyo watatuokoa miaka nenda miaka rudi?

mwanakijiji
03-11-2010, 08:44 AM
Kwa muda mrefu sasa nimeanza kuona mambo fulani makubwa mawili yakitokea inapokuja huduma ya afya.

a. Magonjwa mbalimbali ambayo awali yaliweza kutibiwa katika hospitali zetu yanaanza kupelekwa India. Mtu kamwagiwa tindikali anapelekwa India, mtu anaumwa meno anapelekwa India, mtu kavunjika mguu hadi aende India. Nakumbuka zamani kubwa ilikuwa ni masuala ya moyo. Sasa hivi imefikia hata regular check up inafanywa India, japo zamani tulikuwa tunakimbia hata Nairobi na kwa sisi wengine tunaenda Ndanda au Peramiho.. au hata Bugando. Tumefikaje hapa?

b. Kwa kadiri ya kwamba tunaendelea kutafuta njia mbadala ya kupata tiba na hasa kwa kadiri ya kwamba tunaendelea kuwalipia watawala kwenda kufanyiwa check up na tiba ya magonjwa ya aina yote nje ya nchi, watu hawa hawatofikiria kamwe kuboresha huduma ya afya ya nchini na kuileta kwenye kiwango cha juu cha kimataifa. Zaidi ya yote wataendelea kufungua cliniki na vituo vya afya lakini hawatofikiria kuanzisha kitu kama National Children Hospital au kuigawanya Muhimbili kuwa Muhimbili Healthy Systems badala ya sasa walivyoifanya kuwa tu National Hospital (whatever this means!). Je, kwa kuendelea kuwalipia hawa kana kwamba ni "haki" hatuoni kwamba tumewapa kibali cha kufikiria suala la afya kwa Watanzania kama ni suala "letu" kuliko "lao" kwani wao hawana wasiwasi wapi watatabiwa na nani atawalipia wakiumwa?

Je ipo haja ya kuangalia upya utaratibu wa kuwagharimia viongozi mbalimbali kwenda nchi kwa uchunguzi wa kawaida? Je, tukitaka uchunguzi wa kawaida wote ufanyike nchini yawezekana wakaona uharaka na ulazima wa kuupdate our medical and health facilities?

Ni kwa namna gani suala la afya linaweza kuwa kwenye ajenda ya mwaka huu iili kuweza kuwalazimisha wanasiasa wetu waanze kufikiria hayo mambo mawili hapo juu na kutuongoza kuelekea mabadiliko ambayo yatabadilisha mwelekeo wa sekta yetu ya afya na kuiinua?