PDA

View Full Version : Sumaye kajichongea?



mwanakijiji
03-16-2010, 07:46 PM
Sadick Mtulya (Mwananchi)

KAULI ya Waziri mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye imewachefua wanasiasa na wasomi huku Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia akisisitiza kwamba watu wanaotakiwa kushitakiwa ni pamoja na yeye.

Juzi, Waziri Mkuu mstaafu Sumaye Pamoja na mambo mengine akizungumza na waandishi wa habari alitaka wote waliohusika katika mchakato wa ununuzi wa ndege ya rais na rada washtakiwe.

Pia, alisema endapo sheria ya kutenganisha siasa na biashara itapitishwa, utekelezaji wake utakuwa mgumu.

"Nia ya kutaka kuwepo sheria itakayotenganisha siasa na biashara ni nzuri, lakini utekelezaji wake utakuwa ni mgumu kulingana na mazingira yalivyo lakini utafanikiwa endapo maadili ya Azimio la Arusha yatarudishwa," alisema Sumaye.

Kufuatia kauli hizo, Mbatia alisema mpaka sasa Watanzania wako njia panda kutokana na mfumo mbaya ulioundwa na CCM na kusababisha mambo mengi kufanyika ovyo.

Mbatia alisema kinachotakiwa ni kuondoa mfumo m baya wa CCM na siyo kujadili matukio ya rada au ndege ambayo yalitokea kutokana na mfumo mbaya.

Akifafanua alisema tatizo la Tanzania sio matukio ila ni mfumo wa kiutendaji na kiutawala na kwamba ili nchi iondokane na matatizo hayo ni kutungwa kwa katiba mpya.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Dk Benson Bana alisema pamoja na kwamba wazo la ununuzi wa ndege ya rais na rada lilikuwa zuri, lakini halikuzingatia hali ya kiuchumi, mahitaji pamoja na vipaumbele vya nchi.

“Rada na ndege ya rais yataendelea kumsuta Sumaye pamoja na viongozi wengine wa awamu ya tatu waliyofikia maamuzi ya kununua vitu hivyo,” alisema Dk Bana na kuongeza;“ Walicholalamikia wananchi sio tu gharama kubwa ya ununuzi wa ndege na rada ila ni je ulikuwa wakati muafaka wa kununua vitu hivyo,? alihoji

Kuhusu wataalamu, Dk Bana alisema kuna wakati wanasiasa wanawashinikiza kufanya mambo kinyume na utaratibu na kwa matakwa yao.

“Ni jambo ambalo lipo wazi, kuna wakati wanasiasa huwashinikiza na hata kupuuza ushauri wa wataalamu sasa leo ukisema wa kulaumiwa ni wao

ni jambo la kushangaza. Katika hili, serikali kwa namna yoyote ile haiwezi kulikwepa suala hili,” alisema.

Hata hivyo , Profesa Mwesiga Baregu akizungumza kwa njia ya simu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine(Saut) aliungana na wito wa Sumaye wa kutaka wote waliohusika katika mchakato wa manunuzi wa vitu hivyo washitakiwe.

“Itakuwa ni hatua nzuri kwa serikali kuanza kuchukua hatua ya awali ya maamuzi ya kuwafikisha mahakamani watu wote walihusika katika mchakato wa manunuzi wa rada na ndege ya rais,” alisema Profesa Baregu

Profesa Baregu alisema serikali isipofanya hivyo, itazidi kuwavunja moyo Watanzania.

“Baada ya serikali na Bunge kusimamisha Richmond na ikishindwa kusimamia ipasavyo rada na ndege ya rais, itawavunja moyo Watanzania,” alisema.

My Take:
Binafsi nilikuwa nashangaa hilo hilo.. maana alivyokuwa akizungumza alikuwa anazungumza kama wakati haya yote yanafanyika yeye alikuwa out of body.. na siyo sehemu ya maamuzi hayo ya serikali. Na akiwa mshauri mkuu wa Rais inaonekana hakuwa tayari kusema wakati wowote kuwa alimshauri Rais kitu chochote tofauti isipokuwa kukubaliana naye.