mwanakijiji
03-23-2010, 06:46 PM
Hadija Jumanne (Mwananchi)
WALINZI watatu wa kampuni ya Full Security Guard wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka mawili, likiwemo la kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo kompyuta ndogo kwenye ofisi ya rais mstaafu, Benjamin Mkapa.
Watuhumiwa hao ni Jackson Mbawala, 23, Kamando Athuman, 26, na Asha Sultani, 35, na jana walifikishwa Mahakama ya Wilya ya Ilala.
Hii ni mara ya pili kwa ofisi hiyo ya rais wa serikali ya awamu ya tatu kuvunjwa na kuibwa kompyuta. Katika tukio la kwanza, watu wanne walifikishwa mahakamani kwa kosa la kuvunja na kuiba kompyuta mbili kwenye ofisi hiyo iliyo Mtaa wa Ghana, Upanga jijini Dar es salaam.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda jana, mwendesha mashtaka wa polisi, Daniel Buma alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Machi 17, mwaka huu.
Buma alidai kuwa watuhumiwa hao waliiba televisheni moja yenye thamani ya Sh2.2milioni, keyboard moja ya kompyuta yenye thamani ya Sh 600.000 na monitor power yenye thamani ya Sh480,000, vyote vikiwa mali ya ofisi ya rais huyo mstaafu na vikiwa na thamani ya jumla ya takriban Sh3.2 milioni.
Buma aliendelea kudai kuwa shtaka la pili ni uzembe wa kuzuia wizi huo usitokee kwa kuwa washtakiwa hao ni walinzi.
Washtakiwa hao walikana makosa yao na kesi hiyo itatajwa tena April 15. Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.
Katika hatua nyingine, wakazi wa Tabata Msimbazi jijini Dar es Salaam, Dhoulkefly Abdallah (29) na Asha Kiluvya (32) wamefikishwa mahakama kujibu shtaka la kukutwa na gramu 3,990 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya Sh99.7 milioni.
Mwendesha mashtaka wa polisi, Mussa Gumbo alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo Machi 20, mwaka huu saa 6:00 mchana eneo la Tabata Msimbazi.
Gumbo alidai kuwa watuhumiwa walikamatwa na kukutwa na dawa hizo wakiwa katika hatua za kuzisafirisha.
Hata hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kusema chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Washtakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande babada ya upande wa mahakama kudai kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kesi hiyo itatajwa tena April 6, mwaka huu.