PDA

View Full Version : Kukuku Hadija yule.. kwako wapi?



mwanakijiji
03-25-2010, 10:28 AM
Well.. kuna michezo mbalimbali ya utoto ambayo ilikuwa ni burudani, vituko na wakati fulani ilizaa urafiki wa kudumu sana. Michezo ambayo watoto wetu leo hii wanaweza kuona kuwa haina maana tena na wamebakia kucheza na computer, TV na gameboards..

Kombolela
Kioo kioo
Ukuti ukuti
Kuruka kamba
Hiki na Hoko
Namtafuta rafiki
Tiari bado (mchezo huu ungepigwa marufuku!!!)
Kitambaa changu cheupe
Tukuone maringo yako!
Watoto wangu eh

Upi uliupenda na kwanini?

Matigari
04-03-2010, 06:24 PM
Nangu kwa nini wapige marufuku Tari bado? Au unaogopa Overage kids watatokomea kabisa? Au ulikuwa unaucheza vibaya? Kule Lindi mchezo wa kujipikisha unaitwa madange.

Nilipata kusoma shule ya msingi mjini Musoma, ( darasa la nne) tulikuwa tunacheza mchezo mmoja unaitwa choko, hiyo choko inafananan kidogo na baseball, sijui kama bado watoto wanacheza au la. anayefahamu tafadhali anikumbushe.

Oh kujibu swali lako nilikuwa napenda sana ukuti ukuti, na kidari ( Tag you are it)