mwanakijiji
03-26-2010, 06:45 PM
Na Kyalaa Seheye (Global Publishers)
http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1269589518_ijumaafrontpage.jpg
Supastaa katika tasnia ya filamu nchini Steven Charles Kanumba ‘The Great’ anadaiwa kuwa katika wakati mgumu kufuatia mama yake mzazi, mama Kanumba, kumjia juu akimtaka aachane na mademu masupastaa na kwenda kusaka ‘jiko’ kwenye asili yake, Shinyanga, Ijumaa limeinyaka hiyo.
Akizungumza na gazeti hili, mhabarishaji mmoja (jina tunalo wenyewe) alidai kuwa, mama Kanumba amekuwa akipata presha ya mara kwa mara anapoyachungulia magazeti Pendwa na kuona mwanaye ‘akilidi’ kwa habari za kubadili mademu hasa ikichukuliwa kuwa yeye ni mlokole.
Mhabarishaji huyo akendelea kumwaga kweupe kwamba, mbali na mama mzazi huyo mwenye maskani yake, wilayani Temeke jijini Dar, baba mzazi wa msanii huyo, yaani mzee Charles Kanumba ambaye maskani yake ni Shinyanga ‘Shy’ wote kwa pamoja wamemkomalia kijana wao huyo wakitaka aachane na kubadali ‘akina mama’ hao ambao wanasababisha ukoo kuchafuka wakati wao wazazi wamemlea katika maadili mema.
Aidha, ikadaiwa kuwa, mama huyo alimwambia Kanumba kama anaona kuna mwanamke mwema miongoni mwa hao anaotoka nao kwenye magazeti basi aamue kuchukua jumla kwa kuchumbia na hatimaye ndoa.
“Mama yake hana neno, anasema amemlea mwanaye kwa maadili, sasa anapoona kila kukicha ana demu mwingine anaumia kama mzazi. Lakini akampa chaguo, kama anaona kuna msichana mzuri kati ya hao anaotoka nao, basi aseme ili ipelekwe posa na hatimaye ndoa ifungwe kuliko ilivyo sasa, leo na Wema, mara kesho na Nargis, mara anasikia mwanae sasa anabanjuka na Sylvia, anaumia kama mzazi,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, wakati mama akidaiwa kusema hivyo, hivi karibuni madai yanasema kuwa baba wa msanii huyo alimuita mwanaye huyo Shinyanga na kumwambia suala la kuoa huku akimsisitizia kwamba, anataka kumuona mjukuu wake kabla hajaenda kwenye makazi ya milele.
Aidha, alimwambia kuwa, kitendo cha kuoa ndicho pekee kitakachomtoa mwanaye huyo katika skendo za kutoka na warembo ambazo zinamkabili kwa sasa.
“Hivi juzi tu ametoka Shinyanga ambapo aliitwa na baba yake mzazi na alimwambia suala hilo hilo la kuoa ili kuepukana na skendo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kujaza madai haya kwenye makabrasha yake, Ijumaa lilimwendea hewani Kanumba na kumpa ‘ei bii sii’ ambapo alikiri kukumbwa na ‘kadhia’ hiyo kutoka kwa wazazi wake wakimtaka aoe.
“Ni kweli kabisa, mama kila siku ananiambia nioe kwa kuwa nina umri wa kutosha na yeye anaona uwezo wa kumudu kukaa na familia ninao, ni ushauri wamenipa, japokuwa kashfa pia zimechangia kwa kiasi fulani,” alisema nyota huyo wa filamu nchini.
Akaongeza kuwa, baba yake mzazi naye alimwita hivi karibuini na kilio chake kikubwa ni kutaka kumwona mjukuu wake kabla hajatangulia mbele za haki.
”Baba naye aliniita na kikubwa ni anataka kuona mjukuu wake kabla hajatangulia mbele ya haki na alisema umri umefika na kunishauri kama nitaoa nitaepukana na skendo za ngono katika vyombo vya habari kila kukicha ambazo zinawakwaza. Hilo nakiri kwani hata Shinyanga nimetoka wiki mbili zilizopita,” alibainisha Kanumba
Hata hivyo, alisema kwamba ushauri wao ameupokea na ameuona una maana kubwa katika maisha yake lakini kubwa linalomuumiza kichwa ni kwamba, yeye hayupo tayari kufanya unganiko na mwanamke yeyote kwa sasa.
“Mimi sijawa tayari kuoa kwa sasa, japo wazazi wanasisitiza. Ni kweli nampenda sana mama yangu na najua anaumia sana ila sijawa tayari,” alisema.
Hata alipotakiwa atoe sababu zinazomfanya asiwe tayari kuweka ‘jiko’ ndani, msanii huyo ‘stering’ wa filamu ya Family Tears alishindwa kufafanua na kuishia kusema: “sijawa tayari kwa sasa.”
Mademu ambao wamakuwa wakidaiwa kutoka na Kanumba toka alipoanza kung’aa kwenye gemu ni Wema Isaac Sepetu ambaye kwa miaka takribani miwili wamekuwa gumzo kwenye ‘nyuzi’ kuhusu uhusiano wao. Waliparaganyana mwaka juzi (2008) kila mmoja akashika hamsini zake.
Haikupita muda mrefu ikaja semekana kuwa, staa huyo anatoka na Miss Dar City Centre 2003 ambaye pia ni Miss Ilala 2003 na Miss Tanzania Namba 3 mwaka huo huo, Nargis Mohamed.
Habari zikadai kuwa, wawili hao waliunganishwa wakati wa maandalizi na mazoezi ya filamu ya Yellow Banana ambayo ilishika chati wakati fulani hapa Bongo.
Siku hazijakatika ikajadaiwa kuwa, wawili hao wametemana na kwamba, Kanumba ameamua kuwa ‘singo’ (hataki demu) hali ambayo huenda ilipokelewa kwa mikono yote na familia yake.
Lakini ‘shetani’ mkubwa, Kanumba huyo huyo siku ya siku ‘akaapia’ (akaonekana) kwenye magazeti pendwa akidaiwa sasa anatoka na Miss Ilala 2009, Sylvia Shally
Awali, Kanumba alikuwa akikanusha lakini ilifika mahali akabambwa ‘laivu’ na hivyo kukosa nguvu ya kujitetea kwamba wao si wapenzi.
Hadi tunakwenda mitamboni, habari za mjini kuhusu mastaa ni Kanumba na Sylvia, Kanumba na Sylvia.
Ni kweli inabidi aoe hata kama mwandishi wa habari hii angekuwa mama angeshauri hivyo hivyo!
SWALI:
Je, mambo yakishindakana ya kupata mke "mwema" mjini ni bora mtu arudi kijijini?