mwanakijiji
03-26-2010, 07:10 PM
http://hakinaumma.files.wordpress.com/2008/08/kikwete-msanii.jpg
Kwa mara nyingine tena inaonekana Rais Kikwete anajaribu kuyakamata mapembe ya CCM baada ya habari kuwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu vimeitishwa mwishoni mwa juma hili na mwanzoni mwa wiki inayokuja. Mojawapo ya vyanzo vya uhakika vilidokeza miezi kadhaa nyuma kuwa kuelekea Aprili kuna baadhi ya watu watachukua maamuzi magumu na dalili zinaanza kuonekana.
Matukiio ya hivi karibuni hasa kitendo cha Rais Mwinyi kudai kuwa yeye hakuliua Azimio la Arusha kimeacha moja kwa moja lawama kwa Rais Mkapa na sasa Rais Kikwete. Tutarajie nini?
a. Kwanza CCM inaweza kuanza kulilia Azimio la Arusha kuwa ni "lake". Hivyo, hata kama hawaliamini watajaribu kuwakatisha watu wengine na vyama vingine kutolitumia au kulidai. Watasema ni Azimio la CCM na hivyo bado wanalitambua.
b. Tusitarajie chama kujisafisha kwa sababu kwa muda mrefu wamekana kuwa chama ni kichafu. Wameendelea kusema kuwa CCM ni "safi" kwa hiyo tusitarajie matukio ambayo tutayaita kujisafisha. Zaidi itakuwa ni "mabadiliko tu muhimu kuelekea uchaguzi mkuu".
c. Suala la wagombea binafsi linawasumbua sana na kama Taifa tusikubali hata kidogo uchaguzi uahirishwe kwa sababu ya uzembe wa serikali ya CCM kutii mahakama. Uchaguzi ni lazima ufanyike kama ilivyo Katiba na sheria lazima ifuatwe. Wagombea binafsi watakuwepo.
d. Wizi wa mabilioni ya fedha ambao unadaiwa kufanyika kwenye mabenki kadhaa nchini (inadaiwa zaidi ya bilioni 300) miezi michache kuelekea uchaguzi mkuu unatukumbusha wizi kama huo huo uliotoka muda mfupi kabla ya uchaguzi wa 2005. Japo kuwa taarifa zinadokeza wizi umetokea karibuni lakini uwezekano mkubwa ni kuwa wizi utakuwa umetoka robo ya mwisho ya 2009.