mwanakijiji
04-02-2010, 06:47 PM
MADEREVA WAZEMBE WAONYWA
Na Mohammed Mhina,
wa Jeshi la Polisi
DAR ES SALAAM IJUMAA APRILI 02, 2010. Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kimewaonya vikali madereva wote watakaoendesha magari yao kwa uzembe na kusababishwa ajali kuwa watafutiwa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kutumia sheria za SUMATRA.
Hayo yamebainishwa na Kamanda mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamisna Msaidizi Mwandamizi (ACP) Mohammed Mpinga, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kubainisha mikakati walioiweka katika kupambana na ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha siku kuu za pasaka.
Kamanda Mpinga amesema kuwa wakati wa siku zote hizi watu wengi watakua na pilikapilika za hapa na pale na wengine kutumia siku hiyo kwenda katika kumbi mbalimbali za burudani kwa ajili ya kunywa pombe na kulewa kupita kiasi.
Amesema kuwa Askari wote wa kikosi hicho hawatapunzika na watakuwa kazini kuhakikisha kuwa hakuna Dereva ama mtumiaji mwingine wa barabara atakayeendesha vunja taratibu na sheria za ulama barabarani na hata kusababisha ajali kwa uzembe ama kutokana na vitendo vya ulevi.
Kamanda Mpinga amewataka Madereva na watumiaji wengine wa barabara wakiwemo waendesha bajaji, pikipiki, baiskeli, maguta, mikokoteni na wale waendao kwa miguu, kujidhari na kujiepusha na vitendo vyovyote vitakavyopelekea ajali.
“Tunawataka pia Madereva wote wa mabasi yaendayo mikoani, na wale wanaofanya safari zao kati ya mkoa mmoja na mwingine, kuacha kabisa kwenda mwendo wa kasi ama kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali”. Alisema Kamanda huyo mpya wa kikosi cha Usalama Barabarani nchini.
Kamanda Mpinga amewataka Makondakta na mawakala wa mabasi hayo, wasiruhusu basi kujaa kupita uwezo wake na kwamba yeyote atakayekaidi na kukiuka maagizo hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine watakaoiga.
Aidha Kamanda Mpinga pia amewaomba abiria na wananchi kwa ujumla kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za siri na za haraka pale wanapoona ukiukwaji wa makusudi wa sheria na kanuni za usalama barabarani, kwani nia ya kila abiria ni kufika salama kule anakokwenda na sio kuishia njiani kwa kusababishiwa majeraha ama kufariki kutokana na ajali za barabarani.
Amesema Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na makachero wa Polisi na wale wenye sale za kawaida, watatawanywa katika maeneo mbalimbali kuhakikisha kuwa ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha mfululizo wa siku hizi za mapumziko zinakoma.
Amesema tayari Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi hapa nchini wameagizwa kuhakikiksha kuwa wanawasimamia kwa karibu askari wote waliochini yao ili kuwadhibiti madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuona kwamba havileti madhara ama kusababisha kero na usumbufu kwa watu wengine.
Uwegeshaji wa magari usiozingatia taratibu ama kupakia abiria pasipo na kituo, hasa kwa mabasi ya miji mikubwa, ni mambo ambayo hayatapewa nafasi kabisa katika kipindi hiki.
Amewaomba wananchi na abiria kutosita kupiga simu kwa kutumia namba 0732 928723 au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia simu zao za viganjani kwenda kwenye namba 0767 750198 ili Polisi wachukue hatua.
Naye Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ACP Abdallah Mssika, amewa kumbusha wananchi kutokuacha nyumba zao ama mali nyingine pasipo na uangalizi wa kutosha ama kuacha milango wazi ama kuwaachia watoto wadogo ili kuepuka wezi kutumia nafasi hii kwa kuiba.
Amewakumbusha pia wazazi na walezi kutowaacha watoto ama vijana wao kwenda matembezini ama kwenda kuogelea kwenye fukwe za maziwa na bahari pasipo uangalizi wa watu wazima ili kuepuka watoto hao kuzama na kufa maji ama kunasa kwenye matope.
Hata hivyo Kamanda Mssika amesma kuwa tayari Makamanda wote nchini, wameagizwa kuhakikisha wanaweka ulinzi wa kutosha katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na kufanya doria katika maeneo mbalimbali katika himaya zao ili kudumisha usalama wa wananchi pamoja na mali zao hasa katika kipindi hiki cha mapunziko ya muda mrefu.
Amesema Jeshi la Polisi limejipanga vema kuhakikisha kuwa Wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu.
Lakini pia Kamanda Mssika ametoa angalizo na tahadhali kwa wazazi na walezi kutowaachia watoto wadogo kwenda katika kumbi za sinema zisizo rasmi na kuangalia picha zisizo na maadili kwani picha hizo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika mmomonyoko wa maadili kwa vija wetu.