mwanakijiji
04-05-2010, 08:02 PM
Sadick Mtulya
MBUNGE wa Jimbo la Kahama (CCM) mkoani Shinyanga, James Lembeli ameibuka na kusema kundi la mafisadi ndani ya CCM bado linaendesha propaganda chafu ili kuwaondoa katika chama hicho, wabunge wote waliojipanga kupambana na vitendo vya ufisadi ndani ya chama hicho.
Kauli ya Lembeli inakuja wiki moja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe ambaye naye alikuwa katika kundi la wapambanaji, kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ), kwa kile alichodai CCM imegeuzwa gulio la kila mtafuta cheo na utajiri pamoja na kugeuzwa ngome ya mafisadi kwa lengo la kuficha maovu yao.
Baadhi ya wabunge waliojipanga kupambana na vitendo vya ufisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Aloyce Kimaro (Vunjo), James Lembeli (Kahama) Lucas Selelii (Nzega) na Dk Harison Mwakyembe(Kyela).
Wengine ni Beatrice Shellukindo (Kilindi), Michael Lekule Laizer (Longido) na Christopher Ole Sendeka (Simanjiro) Akizungunza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Lembele alisema kuna kundi la watu limetumwa katika majimbo kadhaa ya wabunge ili kufanya propaganda kwa lengo la kuhakikisha wabunge hao hawarudi Bungeni.
"Kundi la mafisadi ndani ya CCM bado limedhamiria kutuondosha katika chama wabunge tunaopambana na vitendo vya ufisadi ndani ya chama.
"Tayari kuna kundi la watu maalumu limetumwa kupita katika majimbo ya wabunge wanaopambana na vitendo vya ufisadi ndani ya CCM na kufanya propaganda za uongo ili kuhakikisha haturudi tena bungeni,’" alisema Lembeli.
Lembeli ambaye pia ni mmoja wa wabunge wanaopambana na ufisadi, alisema mafisadi hao wanatumia rasilimali zao ikiwemo vyombo vya habari kuwachafua wabunge hao. Alisema vyombo hivyo vinatumika kupotosha hali halisi ilivyo ya kisiasa na kimaendeleo katika majimbo ya wabunge hao.
"Hakuna mbunge aliyemilikishwa jimbo, lakini kutumia mbinu chafu ikiwemo kupotosha ukweli wa hali halisi ilivyo katika majimbo ya wabunge sio uadilifu na ni vitendo vya kukemewa na Watanzania wote wanaoitakia mema nchi hii," alisema Lembeli.
Lembeli alitoa wito kwa wananchi kuwa makini, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Oktoba na kwamba wajiepushe na wanasiasa uchwara, waliofilisika kisiasa ambao sio waadilifu.
"Ninaelewa mikakati ya mafisadi ni kuhakikisha wapambanaji hawarudi bungeni, hivyo ninawataka wananchi kuwa makini na propaganda chafu katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Oktoba na wajiepushe na wanasiasa uchwara, waliofilisika kisiasa kwa kuwa sio waadilifu na hawalitakii mema taifa hilo na wapo kwa maslahi yao binafsi,"alisema Lembeli.
My Take:
Kama hawa jamaa wanataka kutoka CCM watoke tu wasiwasingizie mafisadi! haiwezekani mafisadi wawe na nguvu kiasi hicho!