PDA

View Full Version : Na yupo "Nabii Tito".. utacheka hadi ulie...



mwanakijiji
04-06-2010, 07:36 PM
http://www.youtube.com/watch?v=WisdGYaPKAo&feature=player_embedded

http://www.youtube.com/watch?v=07RcoY8PM5s&feature=player_embedded

duh.. huyu nabii sijui kama ndiyo "nabii yule"!!

Palipina
04-07-2010, 06:13 AM
Wagonjwa wa akili wapo wengi. Huyu angekuwa kwenye nchi hizi za ulimwengu wa kwanza angeonja joto ya jiwe kwa vyombo vya dola. Hata wale wanaomkataa mungu hawafanyi upuuzi huu. Asitegemee kupata umaarufu kwa kufanya mambo ya kijinga.

mwanakijiji
04-07-2010, 08:08 AM
Halafu anatangaza tiba na kuwashauri watu mambo ya kidaktari..halafu bado anaachwa tu..

Steve Dii
04-07-2010, 08:53 AM
What a funny dude.... lol, kilichonichekeza zaidi ni hiyo 'loop' kwenye loudspeaker... na jinsi anavyopiga fegi!! ama kweli vituko haviishi.

Bongo tuna muda mwingi kweli wa kupoteza aise... check watu wanavyorundikana, na hapo ni downtown ambapo angetakiwa asipate hata mtu mmoja wa kumsikiliza... maana ''kila mtu anashika time yake'' badala yake watu wanarundikana... polisi nao sijui wako wapi kwa mtu kuweka kipaza sauti kwa muda wote huo bila hata ya kutiwa kibindoni na kutembezwa kwa kucha kwa kupigia watu kelele!!

Sofia
04-07-2010, 09:32 AM
Mtu kama huyo kwake ni motoni tu! yawezekana ndio uhuru wenyewe huo wa maoni sijui na habari. Siku akitokea fyatu mwingine akianza kuhubiri mengine watu wataanza kulalamika.

Wacha
04-07-2010, 01:24 PM
Watu watamkumbuka JK Nyerere RIP. Huyu anakunywa pombe hadharani yaani sheria zinavunjwa na waliopewa dhamana hawana habari whats going on. Swala muhimu kwa nini kuna watu wengi ambao hata kipato chao hakijulikani je, vyombo vya dola viko wapi? Kazi waliyopewa wanaifanya kama inavyotakiwa? What type of a nation are we building?

mwanakijiji
04-07-2010, 07:28 PM
Wacha.. nani kasema tunajenga taifa? tulishaacha kujenga taifa siku nyingi tu...

Steve Dii
04-08-2010, 12:02 AM
mtanisamehe wakuu... pamoja na kwamba inakashifu dini na kuudhi kwa kelele, haki ya nani tena, hii kitu inachekesha kuliko nilivyofikiria!! Nipo kibaruani leo, basi kila mara nikikumbuka tu hii kideo mbavu nilikuwa sina! Nimekuja kuangalia tena na ninazidi kugundua more funnier things ndani yake...! May be I was wrong even to say that watu wamerundikana bila kazi wakimsikiliza... may be they found it funny just like I currently am.

Steve Dii
04-08-2010, 12:11 AM
eti ukinywa usipoteze network!!!! lol

mwanakijiji
04-08-2010, 12:43 AM
ila jamaa ananifurahisha kweli halafu anathibitisha kile nilichowahi kukisema tunapenda mambo mepesi mepesi kweli.. jamaa kwa vile anazungumza kwa sauti na jazba watu hawataki kumpinga wanaona watakuwa wanajibishana naye..