PDA

View Full Version : Cheche kuelekea Uchaguzi 2010



kadushik
04-11-2010, 04:06 PM
Mwaonaje tukichangia kijarida chetu cha Cheche wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu, naona kijarida hicho kina uwezo wa kuwa baragumu tosha kwa wengi hasa walio mijini na kwa pasenti fulani katasaidia vijijini, haya shime jamani kwani vitani hatuchaguliani silaha.....wenzetu wana silaha yao kubwa ambayo ni fedha .....kisukuma wanasema "Ngosha atahamagwa"

Ach-F
04-11-2010, 04:48 PM
kadushik

wazo zuri wa Harambee ya kuchangia kijarida cha Cheche, nafikiri huu ni wakati muafaka wa kuanza kupata michango kutoka kwa wenye uchungu na nchi yao na mimi binafsi naona kuna haja ya kuanza kuchangia na kutoa. Je, wachapishaji wa kijarida wameweka mikakati ipi? Kitakuwa kinatoka mara ngapi kwa mwezi?