PDA

View Full Version : Akatwa shingo kwa waya uliotegwa!



mwanakijiji
11-23-2008, 07:34 PM
Kaka wa aliyeuawa kinyama Dar azungumza

2008-11-22 16:59:28 (Nipashe)
Na Emaanuel Lengwa, Jijini

Hatimaye yule mtu ambaye majambazi yalimuua kinyama majuzi Jijini Dar es Salaam kwa kumkata kichwa yakitumia waya yalioutega barabarani, ametambuliwa na mwili wake tayari umeshachukuliwa na jamaa zake na kuzikwa.

Mtu huyo aliuawa eneo la Jangwani barabara ya Morogoro usiku wa kuamkia jana wakati akiwa kwenye pikipiki yeye na jamaa yake.

Bw. Omary Abdul Useja, aliyejitambulisha kama kaka wa marehemu, amesema mdogo wake aliyeuawa jina lake ni Zacharia Abdul Useja, aliyekuwa akiishi eneo la Gerezani mtaa wa Lindi Kariakoo, nyumba namba 21.

Kadhalika, Omary amesema mtu aliyekuwa akiendesha pikipiki hiyo ambaye pia alijeruhiwa na majambazi hayo ni mjomba wao, aitwaye Sululu Awami.

Katika tukio hilo, majambazi yalifanya unyama mkubwa baada ya kutega waya barabarani ambao yaliufunga kwenye nguzo za umeme na yalipoona pikipiki ya akina Zacharia na mjomba wake inakuja, yakauvuta.

Waya huo ulimkata shingo Zacharia na ukamjeruhi vibaya mjomba wake ambaye hadi sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiuguza jeraha.

Akisimulia zaidi tukio hilo, kaka wa marehemu, Bw. Omari amesema baada ya majambaji kutenda unyama huo na kupora, yalitokomea. Akasema dereva teksi yenye namba za usajili T 989 AJX anayepaki gari lake pale Muhimbili, ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kutoa msaada.

Amesema japo mdogo wake hakuweza kuokolewa, lakini mjomba wao aliwahishwa hospitali.

Amesema tayari wamemzika ndugu yao baada ya kupewa kibali cha mazishi chenye namba E 0013771 .

Amesema mpendwa wao walimzika kwenye makaburi ya Kisutu.

``Baada ya kumaliza milolongo yote, hatimaye Zacharia tulimhifadhii jana na sasa tunaendelea kumuuguza mjomba,`` akasema Bw. Omary.

Katika tukio hilo, mjomba mtu ndiye alikuwa akiendesha pikipiki hiyo wakati Zacharia alikuwa amepakiwa.

My Take:
Tumefikia wapi sasa?

Kepa
11-24-2008, 02:41 AM
Unajua ukimfuga nyoka hata kama ni mdogo kiasi gani tarajia lolote. Hawa Tumewafuga wenyewe usishangae kati ya hao majambazi walikuwepo watu tuliowaamini kulinda usalama wa raia, tunawakumbatia hao kumbe ni vijinyoka vichanga. Vikishapevuka ndio kama hivi. Siku hizi majambazi wanatawala hadi barabarani, si kwa vificho tena maana tunawalinda haswaaaa.

Hiki kichefuchefu sijui kitaishaje!!:mad::mad:

Mchungaji Ladslaus
11-25-2008, 08:40 AM
RIP Zacharia Abdul Useja

mwanakijiji
11-26-2008, 02:53 AM
Kuna filamu niliiona ya kijapani ilikuwa na scene ya namna hiyo.. it is terrible to imagine kwamba imetokea katika maisha ya kweli.