PDA

View Full Version : Negotiations



Dua
05-11-2010, 03:18 PM
Wabunge wa Liberal Democrats (LD) nchini Uingereza wamekuwa wakitafakari jinsi ya kuunda serikali ya UK kwa majadiliano makali ambayo yanalenga kubadili mfumo wa uchaguzi nchini humo. Gordon Brown anajiuzulu kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kutokana na chama chake kupoteza wabunge takriban 87.


Hali ya Tanzania haipishani na hali iliyopo UK. Je, serikali ya CCM inaweza kumtosa JK? Kutokana na mikataba mibovu ya madini, EPA, Songas, Richmond , Dowans, TICTS etc licha ile ya upotevu wa fedha BOT nk. Wabunge wa LD wameonyesha kwamba hawajali matumbo yao bali yale ya raia wa UK. CCM ambao wamekuwa wanajali matumbo yao zaidi inabidi kujifunza kitu hapa na kuona haki inatendeka kwenye maswala ya kuliinua taifa katika umasikini uliokubuhu huku wageni wachache ambao ni marafiki wa Jakaya Kikwete wakifaidi keki ya taifa peke yao. Tanzania imekuwa nchi tegemezi kimiujiza wakati inawaruhusu maharamia wachache kuchota hazina ya taifa.