PDA

View Full Version : Msiba Italia



mwanakijiji
11-23-2008, 10:26 PM
ABDALLAH MJUME aka DULLAH au Jr, amefariki leo jumapili asubuhi katika nyumba aliyokuwa akiishi. Sababu ya kifo chake bado haijajulikana,ila taarifa fupi kutoka kwa watu waliokuwa nae inasema kuwa Dullah alikuwa Disco kabla ya kufariki. Wakati huo huo Katibu wa jumuiya ya watanzania anawatangazia watanzania wote wanaoishi Napoli kuwa kutakuwa na mkutano siku ya jumatatu saa kumi jioni kwa ajili ya taarifa kamili ya msiba na mipango ya mazishi,wote mnatakiwa kufika bila kukosa. (INALILLAH WAINA ILAH-RAJ'UN) RIP.

Kepa
11-24-2008, 02:44 AM
Poleni sana wote marafiki, ndugu na wanajumuia ya Watanzania waishio Italy. Kwa kweli hapa duniani tunasafiri, hatujui lini tunafika twendapo. RIP rafiki yetu.

makange
11-24-2008, 04:05 AM
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu malali pema peponi!!
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. AMEN!!