Matigari
06-04-2010, 05:42 PM
Hamjambo Wandugu?
Jana nilimpigia simu rafiki yangu wa siku nyingi aishiye Tukuyu Mbeya. Katika mazungumzo nikamuuliza habari za sehemu iitwayo Ndembela nikimuuliza kama imejengeka au la, karibu na mto Mosya. Akaniambia hapana kwa sababu hakuna mtu aendaye sehemu hizo jioni kwa sababu ya mauaji, hasa ya watoto wadogo. Eti siku hizi watua wanaamini kuwa kuua mtoto mdogo kunaleta utajiri.
Jamani huu umasikini na kutaka kupata utajiri wa haraka utatuponza, inabidi tutafute mikakati ya haraka ya kututoa katika huu umasikini, la sivyo tutaingia katika sehemu mbaya sana kwenye uwanja wa haki za binaadamu.
Kutokana na huyo rafiki, watu wa hiyo sehemu wameacha kufikiria kuwa albinos ndiyo wanaleta utajiri badala yake ni watoto wadogo.
Mwe. Mungu atunusuru na huu ujinga.