PDA

View Full Version : Mawaziri nao wakigoma?

mwanakijiji
11-24-2008, 07:42 PM
Inapotokea kuwa wananchi wanaelekeza matatizo na malalamiko yao kwa Rais na kutaka Rais awasaidie au afanye jambo fulani, yawezekana kuwa Mawaziri aidha hawana uwezo, hawajui wafanyalo au na wao wamegoma?

Ni jinsi gani tunaweza kujenga utaratibu ambao utawafanya mawaziri wawajibike kwa watu?

Kepa
11-24-2008, 08:19 PM

Dawa kuu ni kuhakikisaha tuna magugu/ majani Yanayostahili na yakutosha. Hakuna msalie mtume, mtu akichemsaha au kuvuta miguu kazini hataki kuwajibika sisi ni kuotesha magugu / majani kwenye kibarua chake full stop!!

Kepa
11-24-2008, 08:22 PM
Inapotokea kuwa wananchi wanaelekeza matatizo na malalamiko yao kwa Rais na kutaka Rais awasaidie au afanye jambo fulani, yawezekana kuwa Mawaziri aidha hawana uwezo, hawajui wafanyalo au na wao wamegoma?

Ni jinsi gani tunaweza kujenga utaratibu ambao utawafanya mawaziri wawajibike kwa watu?

Hivi kwani kazi wanazopewa hawaja qualify au vipi? kwa nini washindwe kutimiza majukumu yao? au wamegeuza nchi ni ya baba zao? Wamulikwe wooooteeee out :mad:

Mchungaji Ladslaus
11-24-2008, 10:11 PM
Inapotokea kuwa wananchi wanaelekeza matatizo na malalamiko yao kwa Rais na kutaka Rais awasaidie au afanye jambo fulani, yawezekana kuwa Mawaziri aidha hawana uwezo, hawajui wafanyalo au na wao wamegoma?

Ni jinsi gani tunaweza kujenga utaratibu ambao utawafanya mawaziri wawajibike kwa watu?

Mie sioni kazi/wajibu wa waziri pale wizarani maana tayari tuna makatibu wakuu na manaibu wao pia tuna wakurugenzi wa vitengo mbalimbali na madaibu wao.

Tunahitaji kurestructure mfumo wote wa uongozi hapa Tanzania.

mwanakijiji
11-24-2008, 10:52 PM
Mchungaji hilo litafanikiwa vipi? Leo hii tunaona jinsi Obama anavyotengeneza serikali yake mpya na ana karibu miezi miwili kufanya hivyo. Sisi Tanzania Rais akishachukua madaraka anasiku saba za kuapishwa na zisipite siku 21 kabla ya kuwa na Waziri Mkuu mpya na Baraza la Mawaziri. Sasa katika mtindo huo Rais kweli anakuwa na muda wa kuvet mtu mpya? Ndio maana nadhani wanabakia kurecyle viongozi "wale wale".