View Full Version : Nini kinakuboa/kukufurahisha movie za kibongo?
mwanakijiji
08-27-2010, 10:05 AM
Siku za karibuni nimeanza kuzama katika kufuatilia visa mbalimbali vya masimulizi ya filamu za Kibongo. KUna ambazo zinanivutia na kuna ambazo hata kumaliza siwezi. Najua wengi tuna namna tunavyochukulia kwani kuna wengine ukisema movie za kibongo wanaona kama kituko na wapo wengine ambao wakirudi nyumbani tu kitu cha kwanza ni kuangalia wapi kuna movie mpya na "the Great" katoka na nani.
Wewe mwenzangu ni kitu gani unakipenda au hukipendi kuhusu movie za Kibongo.
NB: KUna movie nitaanza kuzijadili hapa siku chache zijazo nikishamaliza kuziangalia.
monsignor
08-28-2010, 11:27 PM
Kimoja kinachoniboa ni jinsi baadhi kama siyo wengi wa waigizaji wanavyoshindwa kuuvaa uhalisia wa nafasi wanazocheza. Kwa mfano utakuta mtu anaigiza kama daktari , badala ya kujitahidi walau kuuliza kwa matabibu jinsi wanavyofanya baadhi ya shughuli zao kabla hajaingia studioni, utakuta muigizaji anafanya anavyojua au anavyodhani ni sahihi. Kwa tabibu ninapoangalia na kuona jinsi kazi yangu inavyoigizwa na kukosewa waziwazi huwa naboreka sana. Ofcoz sitarajii msanii kuweza kuwa perfect lakini walau ajitahidi kuonesha weledi fulani katika sehemu yake aliyopangiwa kucheza na ikiwezekana director kuuliza kwa wenye taaluma zao jinsi wanavyofanya mambo ili kuepusha makosa yanayoweza kuepukika. Kadhalika kwa nafasi zinazozungumzia fani nyingine mbali mbali huwa kuna mapungufu ya waziwazi yanayofanya movie nzima ipoteze maana na kuonekana kweli waigizaji walikuwa wanaigiza.
MAHESABU
09-21-2010, 01:29 AM
senema nyingi za hapa kwetu zinakosa vionjo na ladha ya kikwetu.....zimejaa maisha yasyo ya kwetu na kukumbatia kusiko kwetu..kweli waigizao wanaangalia soko zaidi lakini soko bila kujali kwako ni utumwa...MAVAZI...MAJINA...UJUMBE...MAZINGIRA N.K
Mkiritimba
01-02-2011, 02:49 PM
Sinema ziko kama maigizo. Ukiiangalia tu mwanzo unajua mwisho wake utakuwaje,ziko soooo predictable. There is no suspense at all!Bora hata cartoons za Fredy Quimby!
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.