View Full Version : Cheche - Kagoda ni ya Kina Rostam!
mwanakijiji
11-25-2008, 08:40 AM
Jipatie nakala yako; na ukipenda kupata kijarida hiki kwenye email, fuata maelekezo ndani ya jinsi ya kujiandikisha.
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/toleo15.jpg
Mpita Njia
11-25-2008, 10:08 AM
Lakini ni kwa nini mamlaka zinajiumauma kutaja hili jambo kwa uwazi? Kinaogopwa nini?
mwanakijiji
11-25-2008, 04:07 PM
Sidhani kama wataendelea kuogopa tena, maana tumewakimbizia kuku, tumewakamatia, na kuwachinjia.. wao wanatakiwa wapike tu!
Sidhani kama wataendelea kuogopa tena, maana tumewakimbizia kuku, tumewakamatia, na kuwachinjia.. wao wanatakiwa wapike tu!
Na ili wasitupige changa la macho, tunasisitizia kuwa baada ya kuwapika tutaonja mchuzi tujue kama ni wa kuku au walibadilisha wakawapika 'NDEGE- SHYCOM' ??
mwanakijiji
11-26-2008, 01:10 AM
nami nakupata vizuri kabisa..
mwanakijiji
11-27-2008, 06:55 AM
mtu akisoma hiyo habari maalum ya "Cheche" halafu akasoma ile thread juu ya "Usalama wa Taifa" na mtu huyo anauwezo wa kujumlisha 2 + 2 basi hata kama watafanya watu 100 iwe kijijini au mjini jibu lao litakuwa ni lile lile..
mwanakijiji
11-27-2008, 09:52 AM
Mbona watu wamejificha huku kwenye "Cheche" hawatoki? Kwa wale wageni matoleo yote ya "Cheche" yatakuwa hapa kuanzia kesho ili kuweza kujua tumetokea wapi. Kwa wale ambao wanapenda kupata kijarida hicho kwenye email zao, wamuandikie mhariri kwa anauni iliyomo humo.
Monica
11-27-2008, 09:57 AM
Eti nasikia ndio wameshiliklia uchumi wa nchi huvyo wakikamatwa uchumi wa nchi utayumba. Miye sikuelewa hilo. sasa bank kuu inahaja ya kuwepo?
Mpita Njia
11-27-2008, 04:43 PM
Eti nasikia ndio wameshiliklia uchumi wa nchi huvyo wakikamatwa uchumi wa nchi utayumba. Miye sikuelewa hilo. sasa bank kuu inahaja ya kuwepo?
Monica, nionavyo mimi ni kuwa hawa jamaa hawajashika uchumi, bali wamezishika akili zetu, ndio maana tunapatwa na hofu sana kila wanapotajwa
mwanakijiji
11-28-2008, 08:51 AM
Eti nasikia ndio wameshiliklia uchumi wa nchi huvyo wakikamatwa uchumi wa nchi utayumba. Miye sikuelewa hilo. sasa bank kuu inahaja ya kuwepo?
Nadhani hawa jamaa kuna kitu wamekishikilia zaidi ya Uchumi.
Mr. XXX
11-28-2008, 06:25 PM
Hivi Rostam kakuudhi nini wewe? Wakati serikali inasema haijui mmiliki wa Kagoda wewe unakuja na habari zako hizi. Stori inavutia lakini kumbuka hawawezi kukata tawi walilokalia!
Mkongwe
11-30-2008, 07:19 PM
Nimekupata Mwanakijiji. Sasa sijui wanapata kigugumizi gani kuwakamata wahusika
jatropha
01-02-2009, 06:07 PM
Ndugu mwanakijiji,
naomba nitumie jarida la Cheche linalohusu Kampuni ya KAGODA
Lakini ni kwa nini mamlaka zinajiumauma kutaja hili jambo kwa uwazi? Kinaogopwa nini?
Asalaam Aleykum Mpita Njia.... na wala usijikwae maana bado safari inakuhitaji kwa kasi ile ile.. Nimeguswa na swali lako na mimi ninajiuliza kwamba labda hizi mamlaka ni "Jino la Pembe ambalo katu si dawa ya pengo", kama wanaufahamu huu. Labda tena nami niulize kwamba yote haya yamesababishwa na "Kifo cha mdomo!!!? Mate kutawanyika!!!!...."::rolleyes:
dickabudi
01-28-2009, 09:10 AM
Please lets know the report from BRELLA and the previous report of Mwanakijiji on owners of KAGODA
dickabudi
01-28-2009, 09:13 AM
Please lets know the report from BRELLA and the previous report of Mwanakijiji on owners of KAGODA
Mwanakijiji kindly I am very anxoius to know the owners given by BRELLA Chief how do they relate to the Aziz Family
Becaouse we tend to believe that KAGODA belongs to Aziz Family
The names of Kagoda as per BRELLA Chief differs from Cheche we need clarification for this
Mpita Njia
01-28-2009, 11:15 AM
Mwanakijiji kindly I am very anxoius to know the owners given by BRELLA Chief how do they relate to the Aziz Family
Becaouse we tend to believe that KAGODA belongs to Aziz Family
Pekua kwenye archives za majarida ya Cheche, utakutana na jarida moja ambalo liliandika habari hii kwa undani. Kila la heri
Mpita Njia
01-28-2009, 01:39 PM
Asalaam Aleykum Mpita Njia.... na wala usijikwae maana bado safari inakuhitaji kwa kasi ile ile.. Nimeguswa na swali lako na mimi ninajiuliza kwamba labda hizi mamlaka ni "Jino la Pembe ambalo katu si dawa ya pengo", kama wanaufahamu huu. Labda tena nami niulize kwamba yote haya yamesababishwa na "Kifo cha mdomo!!!? Mate kutawanyika!!!!...."::rolleyes:
Lakini, ukiangalia jinsi mchezo unavyochezwa, hizi kesi (kubwakubwa????) jinsi zinavyofunguliwa na watu wanaoshitakiwa, mtu unaweza kuwa unaunganisha nukta na itafika siku utapata picha kamili, hata kama kinachofanyika kinafanyika kwa lengo la kuficha maovu. Huo mcherzo wao ndio unaoweza kutusaidia kupata kujua ni nini hata kilichotokea. Nadhani hata wao wanafahamu kuwa fumbo anafumbiwa mjinga, hivyo kama hizi kesi ni aina ya fumbo, kalaghabao!!!!
hofstede
01-28-2009, 03:08 PM
Mzee MM mbona siku hizi inakuwa tabu sana kupata kijarida yaani kimejificha mpaka mtu u-google (joke). Naomba nitumie na mimi kijarida, marekebisho ya e-mail yangu ntaku-PM
hofstede
01-28-2009, 03:09 PM
Nimeshakiona kijarida mzee MM, Poa
mwanakijiji
01-28-2009, 03:59 PM
Mzee MM mbona siku hizi inakuwa tabu sana kupata kijarida yaani kimejificha mpaka mtu u-google (joke). Naomba nitumie na mimi kijarida, marekebisho ya e-mail yangu ntaku-PM
tuma email kwa mhariri@klhnews.com ndiyo njia ya uhakika zaidi ya kukipata.
dickabudi
01-30-2009, 12:30 PM
Mwanakijiji kindly I am very anxoius to know the owners given by BRELLA Chief how do they relate to the Aziz Family
Becaouse we tend to believe that KAGODA belongs to Aziz Family
The names of Kagoda as per BRELLA Chief differs from Cheche we need clarification for this
The names of Kagoda owners as per BRELLA Chief differs from those provided in Cheche, can we have more clarification from Cheche to see how Government Agency can Cheat
mfumwa
01-30-2009, 03:12 PM
The names of Kagoda owners as per BRELLA Chief differs from those provided in Cheche, can we have more clarification from Cheche to see how Government Agency can Cheat
Waliposema EPA sio hela za Serikali, na sasa kuna wanaoshitakiwa kwa fedha za EPA, huwezi pata picha ya majina yanayotoka BRELA na ambayo yanatajwa kuwa ndio wamiliki wa KAGODA. Na hao jamaa waliotajwa na huyo mkuu wapo?
dickabudi
01-30-2009, 04:03 PM
Ninachopenda kukijua je majina ya wanahisa waliotajwa na BRELLA wapo? Pia wafanyakazi wa Rostam au Ndugu wa Rostam waliotajwa kwenye cheche ni wapi wamiliki halali hivyo nilipenda Cheche iwatafute na wadhibitishe kweli wao ni wamiliki halali wa KAGODA au la
Napenda kuwa kama TOMASO wa kwenye Biblia kupata mawasiliano ya pande hizo mbili au ushahidi wa wazi kuwa wamiliki waliotajwa na Mkuu wa BRELLA ni uongo hawapo na wameshindwa kupatikana
mwanakijiji
01-30-2009, 04:47 PM
Ninachopenda kukijua je majina ya wanahisa waliotajwa na BRELLA wapo? Pia wafanyakazi wa Rostam au Ndugu wa Rostam waliotajwa kwenye cheche ni wapi wamiliki halali hivyo nilipenda Cheche iwatafute na wadhibitishe kweli wao ni wamiliki halali wa KAGODA au la
Ubishi wa fedha za Kagoda hauko kwenye wamiliki. Soma toleo letu la wiki iliyopita utaona kuwa kujadili wamiliki n.k siyo tatizo kwani kwenye makaratasi, wamiliki wa Kagoda wanajulikana. Sisi tumeenda mbali zaidi kuonesha kuwa hao wawili ni front men wa kundi la watu wengine. Ndiyo maana katika toleo letu linalofuata swali letu siyo "nani mmiliki" bali "nani alichukua fedha benki".
Hilo swali hadi leo hakuna aliye tayari kujibu!
Napenda kuwa kama TOMASO wa kwenye Biblia kupata mawasiliano ya pande hizo mbili au ushahidi wa wazi kuwa wamiliki waliotajwa na Mkuu wa BRELLA ni uongo hawapo na wameshindwa kupatikana
Sisi tumeweka kesi hadharani. Ungeuliza Polisi je mmewahoji hao wamiliki waliotajwa na Brela? Je wamemhoji yule mhasibu (Mwang'onda) aliyetia sahihi yake kwenye fomu za Incorporation za Kagoda? Je wamemhoji wakili wa kampuni hiyo?
Tuna uwezo wa kufanya hayo yote, but then, tutakuwa ni polisi sisi. Sisi tunaonesha mwanga tu wa wapi wao waende, kama hawataki too bad.
jbngatunga
02-10-2009, 12:01 PM
Ndugu zangu watanzania, sheria ifuate mkondo wake wala tusitishike na kauli za kusema kuna baadhi ya mafisadi wakikamatwa eti uchumi wa nchi yetu utayumba, kama kuyumba kiuchumi tulishayumba na sababu ni hawahawa mafisadi! NAMWOMBA RAIS WETU JK ASIMWONEE HAYA MTU YEYOTE KWA NAFASI ALIYONAYO AU ALIYOKWISHA SHIKA KATIKA NCHI HII, KWA SABABU WAO NDIO SABABU YA KUTUFIKISHA MAHALI HAPA! HATUTAKI KULINDANA TENA KATIKA TAIFA HILI! JK kuwa jasiri wa kutotetea mtu yeyote acha wao wenyewe wakajisafishe mbele ya vyombo vya sheria kwa sababu ukifanya hivyo GOD IS GOING TO JUDGE YOU!
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.