PDA

View Full Version : Tunaweza kupanga tarehe ya uhuru wetu?

Mpita Njia
11-25-2008, 11:19 AM
najiuliza hivi nikimaanisha kuwa hivi sasa tu koloni-tunatawaliwa na wenzetu, ambao tuliwachagua wawe viongozi, lakini wameamua kujigeuza kuwa watawala. Kama ambavyo wakoloni wa Kiingereza, Kijerumani na Kiarabu walivyotutawala, na ndivyo ambavyo Chama Cha Mapinduzi kinavyotutawala. Kumbuka, kinaitwa Chama tawala. na ndivyo ambavyo vyama vingine vinavyowania kututawala.
Lakini, majiuliza, hivi tunaweza kuinuka na kuanza kudai uhuru wetu? Akina Nyerere na wenzake hawakuweza kujipangia tarehe ya kupata uhuru, lakini 1960's ni tofauti sana na 2000's. Je sisi tunaweza kujipangia tarehe yetu ya kupata uhuru?

makange
11-25-2008, 01:55 PM

Waswahili wanasema: "Penye NIA pana NJIA"

gashle
11-25-2008, 02:35 PM
Kuna nyakati naona aibu kuitwa Mtanzania kutokana na hali ambayo ndugu zangu Watanzania tunayo... we are so soft hata katika yale tunayopaswa kuwa wakali. Tumezubaa kwa kweli. Ila imani yangu ni kwamba yote yanawezekana, nyakati zinakuja, naam nyakati zipo ambazo tutasimama pamoja na kusema yatosha.

Hatuhitaji Watanzania wote 34 million nne wote kuvaa ujasiri wa kuleta mageuzi nchini. Tunahitaji kiongozi, others will follow, leaders are few ...

Come on Watanzania

magoma
11-26-2008, 07:44 PM

Mi siamini kama wakati unakuja, LINI?? Mi naamini wakati ni HUU tuanze sasa kudai uhuru wetu maana madai sio ya cku moja wakati tunaaanza sasa kufikia muda huo unao kuja tutakuwa tumefikia lengo lkn tukisubiri muda huo ufike ndo tuanze kudai uhuru basi itakuwa too LATE, Watakuwa wamesha chukua chao mapema na kukimbilia uhamishoni kuhifadhiwa na wezi wenzao wa nchi za mbali. TUANZE SASA WITO

mwanakijiji
11-26-2008, 10:14 PM
Wenzangu mmekuwa wapi muda wote huu? Tunachopigania sasa ni hicho, ni haki yetu ya kuwa watu huru na wenye utu wa kweli; Tunachopigania ni kuwa na nafasi ya kufanikiwa katika maisha yetu na kuweza kujenga kweli Taifa la watu walio huru na sawa; tunachopigania ni uhuru siyo toka kwa wageni bali kwa watawala wanaotutawala kama wao wageni!

Kepa
11-27-2008, 01:27 AM
'Wenzangu mmekuwa wapi muda wote huu? Tunachopigania sasa ni hicho, ni haki yetu ya kuwa watu huru na wenye utu wa kweli; Tunachopigania ni kuwa na nafasi ya kufanikiwa katika maisha yetu na kuweza kujenga kweli Taifa la watu walio huru na sawa; tunachopigania ni uhuru siyo toka kwa wageni bali kwa watawala wanaotutawala kama wao wageni!'
MWANAKIJIJI (2008)

Somo naona linakolea Wandugu na Wadada. GET READY>>>>>> GO.........!!!!