View Full Version : Mramba na Yona Mahakamani: Kumkaribia Mkapa?
mwanakijiji
11-25-2008, 05:09 PM
Vyanzo vyote vya ndani vinatonya kuwa kwa vile haiwezekani kumfungulia mashtaka Rais Mstaafu basi wale wote waliokuwa karibu yake na wanaohusika na ufisadi watasimama kizimbani!!
Ach-F
11-25-2008, 11:54 PM
Mramba na Yona lazima sheria ichukue mkondo wake na bado wapo wengi tu ambao ni lazima washitakiwe kwa hujuma ya mali ya Taifa. Edward Lowasa ambaye tangu alipojiuzulu hajafanyiwa chochote kutokana na kulitia hasara taifa. Sheria ya wahujumu lazima ifanye kazi yake.
Kama kweli Jakaya Kikwete anataka urais 2010 ni lazima vigogo wote wachukuliwe hatua na kesi zao kwisha kabla ya 2009. Asitoke mtu hapo.
Ach-F
11-26-2008, 01:53 AM
Pesa zote hizo wanazoiba hawashibi dawa yao ni kuwaweka ndani na funguo kuzitupa bahari ya hindi. Jakaya Kikwete tumia sasa powr ya urais kama unaweza maana rais wa bongo ana nguvu za kiajabu! Bomu hilo liko mikononi mwako usisubiri likupasukie. Eh ehe heheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ati mwenyewe anajiita JK !
mwanakijiji
11-26-2008, 02:15 AM
lakini kuwagusa hawa itaonekana ni kisasi. Je yawezekana kuwa JK ameamua kujitangaza uadui na BM? Kinachonishangaza ni kuwa hili suala lilikuwa linajulikana kabla hata ya uchaguzi wa 2005; Kwanini JK aliamua kumteua Mramba na kumpa Wizara?
Mpita Njia
11-26-2008, 05:58 PM

Mkuu, inaweza kuwa inamaanisha jambo moja tu... upo msemo wa kiswahili, ukiwa unajua huku, mwenzako anajua kule. kama JK alikuwa anajua huku, kuna uwezekano mkubwa kuwa na Mramba alikuwa anajua kule kuhusiana na bwana mkubwa.
Lakini kama hivyo ndivyo, kwa nini wageukane sasa? He nimeuliza swali lilelile!!!!
mwanakijiji
11-26-2008, 06:38 PM
Kama kuna Kugeukana nadhani lazima turudi kwenye Kiwira kupata Clue....
magoma
11-26-2008, 06:49 PM
kwa mtazamo wangu ingawa mi jaji/hakimu mi nadhani kuna watu wanastahili adhabu ya kunyongwa hadi KUFA hadharani maana wamehujumu maisha ya watu hawa jamaa, mambo ya kesi ni magumu na mshangao zaidi kuna eti watu wanajiita mawakili wameenda kuwatetea. unatetea mwizi!!!! oh no hata kaka ni ujira hapa haipendezi proffessionally. ina maana huna uchungu na taifa lako!!!!!!!!!!!!! natoa hoja
magoma
11-26-2008, 07:04 PM
Tunasubiri mzee wa VIJISENTI (CHENGE) NA MZEE MZIMA MKAPA NA MKEWE ANNA, VILEVILE BILA KUMSAHAU MKUU WA TAKUKURU, MWANA SHERIA MKUU. Nakumbuka mthumiwa Mramba aliwahi kutuambia hata kama tutakula majani lakini lazima ndege ya Raisi inununliwe sijui ilikuwa kwa manufaa ya nani, mlipa kodi au mtumia kodi yetu sasa ananyea ndoo keko atakumbuka maneno yake wakati anaongea na waharifu wenzake huko KEKO MAGURUMBASI. Toka MASAKI hadi KEKO na kuvaa ndala mkuu!!!!!!!!!!!!!!!!!! KWELI sheria msumeno.
Mpita Njia
12-01-2008, 02:35 PM
Habari za hivi punde kutoka Mahakama ya Kisutu ni kuwa Mramba na Yona wamerejeshwa tena Keko baada ya hakimu kukataa kuisikiliza kesi yao leo. Hakimu alisema kuwa hakuipanga kesi hiyo leo na alishangaa kuwaona watuhumiwa hao mahakamani kwani hakutoa removal order yo kulitaka jeshi la magereza liwalete watuhumiwa hao.
Ameipanga kesi hiyo kusikilizwa keshoooooooo
My more
12-01-2008, 06:36 PM

Aaah huyu hakimu simuwezi, hivi mahakimu wa aina hii bado wapo Bongo?
Sijui ingekuwaje kama angepewa kesi ya yule Dereva wa daladala aliyeuwawa kwa mtutu. Naanza kuamini Tanzania hapatabiriki.
mwanakijiji
12-01-2008, 07:09 PM
Aaah huyu hakimu simuwezi, hivi mahakimu wa aina hii bado wapo Bongo?
Sijui ingekuwaje kama angepewa kesi ya yule Dereva wa daladala aliyeuwawa kwa mtutu. Naanza kuamini Tanzania hapatabiriki.
Mimi nadhani kama ilivyokuwa kwa yule Hakimu Mkazi mwingine ambaye baadaye aliukwaa Ujaji ndivyo ilivyo kwa hao wa Kisutu. Kumbuka kuwa Mahakama ya Kisutu ndiyo penye ujiko kuliko mahakama nyingine nyingi za chini na hivyo ni jukwaa la kujinadisha Ujaji.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.