mwanakijiji
11-26-2008, 02:05 AM
Bi. Aziza anatoa somo jingine:
Mahitaji:
MCHELE KILO 1
KUKU MKUBWA 1
VITUNGUU MAJI KILO 2
MAYAI 8
SAMLI KILO 1(AU MAFUTA)
VITUNGUU THOMU GRAM 200
TANGAWIZI MBICHI GRAM 50,MDALASINI GRAM 50.
HILIKI GRAM 50
BIZARI NZIMA KIASI
SIKI KIASI
MTINDI PAINT 1
NYANYA KILO 1
ZABIBU KAVU NYEUSI KIASI
Jinsi ya kupika
1-mkate kuku umuoshe umchemshe kwa maji na chumvi mpaka aive,kisha muepuwe.
2-menya vitunguu uvioshe uvikate na uvigawe sehemu mbili.sehemu moja uiweke;sehemu ya pili vikaange mpaka viwe vyekundu kama vya biriani.kisha vichuje uitoe samli yote,vitie ktk sinia uvitandaze ili vipowe kwa kupata upepo.
3-chukua mdalasini,hiliki na bizari utwange pamoja,kisha uchunge unga laini.saga thomu na tangawizi mbichi.saga nyanya.
4-teleka sufuria tia samli ile ile iliyokaangiwa vitunguu halafu utie vitunguu vilivyosalia uvikaange.
vikianza kuiva tia viungo ulivyovitwanga na kuvisaga.(bakisha vitunguu na viungo kidogo).
tia vipande vya kuku,mtindi,siki na supu ya kuku iliyosalia ktk sufuria.acha ichemke nyama pamoja na vitu vyote mpaka ibaki rojo rojo.
5-teleka maji,yakichemka tia mchele.ukiiva utoe uuchuje yatoke maji yote.
6-teleka tena sufuria utie samli kidogo utie na vile vitunguu ulivyovisaga uvikaange.tia mdalasini mzima,kaanga pamoja,tia na ule wali ukoroge koroge ili uchanganyike na viungo.kisha ufunike upalie moto(au utie ktk oven)
7-chamsha mayai yote uyamenye.
8-wali ukeshakauka,lakini itabidi utumie kombe au sahani kubwa itakayoweza kuingia wali pamoja na vitu vyote.
9-kuupakuwa kwake kwanza utatia nusu ya wali ktk hiyo sahani,baadae utatia masalo pamoja na nyama yote,na mayai,kisha utayafunika masalo pamoja na nyama yote kwa wali uliosalia.
mwisho utachukuwa vile vitunguu ulivyovisaga ukavitandaza ili vipowe utavimwaga juu ya wali.
kwa ni kwasababu ya hivi vitunguu ndio maana ukaitwa wali wa asumini.
ukipenda utapambia chembe za zabibu juu yake zabibu hizo ziloweke ili zivimbe.
Karisha mgeni wako mjinome!!