PDA

View Full Version : ~ Altare ya Machozi ~ Na. M.M.Mwanakijiji



mwanakijiji
11-26-2008, 08:27 AM
Sura ya I

?Vivian Tembo, unampokea Charles Mugisha kuwa mume wako wa ndoa, umuenzi na kumtunza, kumpenda na kumlinda katika shida na raha, katika magonjwa na afya mpaka kifo kiwatenganishe?? Padre Amedeus Minja alimuuliza bibi harusi.

?Ndio nampokea!? Vivian alijibu kwa sauti ya upole, lakini iliyonaswa vilivyo na vipasa sauti vya Kanisa la Mtakatifu Joseph Jijini Dar-es-Saalam. Jibu lake hilo lilisababisha mlipuko wa vigelege, hoi hoi, na makofi ambao nusura uziangushe kuta za Kanisa hilo maarufu. Kabla ya chereko chereko hizo kukoma kwaya ya Mtakatifu Joseph iliyokuwa ikiongozwa na Veronica Mwangwi ilirukia na kuanza kuimba kibwagizo chao maarufu cha ?Nimekuchagua wewe, kati ya wanaume wote, uwe msaidizi wangu!? Mara kibwagizo hicho kilipoisha, Padre Minja alimgeukia kijana Mugisha na kumrushia swali hilo hilo.

?Charles Mugisha, unampokea Vivian Tembo kuwa mke wako wa ndoa, umuenzi na kumtunza, kumpenda na kumlinda, katika shida na raha, katika magonjwa na afya mpaka kifo kiwatenganishe? Aliuliza huku akielekeza kinasa sauti upande wa Charles.

Charles alijaribu kufungua mdomo wake na kutoa jibu la ?ndio nampokea?; mdomo haukufunguka. Alijihisi kupatwa na kizungu zungu cha ghafla huku miguu ikimtetemeka kama mianzi ikipigwa na upepo. Alijaribu tena kutamka maneno hayo ya kukubali lakini ulimi wake uligandamana na kaakaa la kinywa chake kama umetiwa gundi ya mbao. Koo lilimkauka na moyo wake ulianza kumwenda mbio huku mdundo wake ukisikika kwa mbali kwenye vipasa sauti vya kanisa hilo. Ukimya mkubwa ulitanda kama ukimya wa kaburi. Hakupiga mtu chafya, wala kujaribu kupigwa mwayo. Wazazi wa bibi harusi, wanawali waliofuatana na bibi harusi wote walikodoa macho kumwelekea Charles, na macho yakawatoka utadhani gololi! Kila mtu alijiuliza ni kitu gani kimemsibu kijana huyo.

Kanisa lilikuwa kimya wakati Charles anatafuta maneno ya kujibu. Padre Minja akaona ajaribu tena kumuuliza kijana huyo aliyevalia suti ya kupendeza ya rangi nyeusi ambayo koti lake lilikuwa na michirizi ya kumetameta ya rangi ya maziwa na kingo zake zikifika hadi magotini. Upande wa kushoto alikuwa amening?iniza ua jekundu la waridi, na miguuni akiwa ametinga viatu vya Armani ambavyo alizawadiwa na rafiki yake toka Italia.

?Charles Mugisha, unampokea Vivian Tembo kuwa mke wako wa ndoa, umuenzi na kumtunza, kumpenda na kumlinda, katika shida na raha, katika magonjwa na afya mpaka kifo kiwatenganishe?? Alirudia tena Padre Minja.

Ndani ya moyo wake na akili zake Charles alikuwa kama birika la chai ambalo lilikuwa likichemsha maji yakachemka na yakiwa tayari kumwagika kutokana na nguvu za msukumo wa joto lake. Alikuwa karibu kupasuka kwa msukumo wa hofu, woga, aibu, hatia, na kila aina ya hisia hasi. Alijaribu kukohoa kidogo kusafisha koo lake. Alimwangalia bibi harusi ambaye wakati huo mdomo wake ulikuwa umebakia wazi kiasi cha kuwa kama mlango unaokaribisha inzi! Charles alimuangalia Vivian na akajaribu tena kutoa kauli ya kukubali. Haikutoka. Alikuwa kama gari lililozima katikati ya reli huku treni likija kwa kasi toka upande mmoja na jitihada zote za kuliwasha zikishindikana.

Vivian aliinua macho yake na kuyagonganisha na ya mchumba wake, mawazoni alikuwa na maswali milioni moja na moja ambayo angependa kumuuliza kimemsibu kitu gani. Alipomuangalia vizuri aligundua kuwa Charles alikuwa amelengwa na machozi na yeye mwenyewe Vivian alijigundua kuwa machozi yameanza kufurika kwenye macho yake na kuanza kufanya michirizi kwenye pande za mashavu yake huku yakiharibu poda, wanja, na vimetameta alivyokuwa amepambwa navyo kwa ajili ya harusi hiyo. Wapenzi hao wawili walijikuta wakibubujikwa na machozi.

Charles alimgeukia Padre Minja na kumwashiria amsogelee ili amnong?oneze kitu.

?Baba Padre, naweza kujibu swali hilo, lakini kabla sijafanya hivyo naomba nafasi ya kuungama kitu kwako na kwa Vivian, tafadhali? Alisema kwa sauti ya upole, ya chini lakini iliyokuwa na uhakika wa kile isemacho. Padre Minja alitingisha kichwa kuashiria amemuelewa. Vivian hakujua Charles amemnong?oneza kitu gani padre huyo, maswali akilini mwake yaliongezeka na kuwa milioni moja na mbili. Padre Minja aliwageukia waumini ambao wote walikuwa kimya wakisubiri kwa hamu kujua ni nini kinaendelea. Waliokuwa wambeya hawakuchelewa kuanza kuzusha uvumi, na wenye simu wakaanza kutumiana ujumbe kuwa Vivian kaachwa altareni!

?Wapendwa katika Bwana!? Padre Minja alianza kuzungumza kwa sauti kakamavu iliyomgutusha kila mtu kanisani humo. ?Tumesikia jibu la bibi harusi, lakini bwana harusi kabla ya kutoa jibu lake, ameniomba twende chemba ili afanya maungamo ya dhati kabla kutoa jibu hilo. Hivyo kwaya itaendelea kuburudisha wakati mimi, bwana harusi na bibi harusi tutakuwa sakristia na pindi tukimaliza tutarudi. Asanteni? Alimaliza huku akiwaongozwa wachumba hao kuelekea kwenye sakristia pembezoni mwa kanisa hilo.

Padre Minja alivuta viti vitatu vilivyokuwa vimekunjwa pembeni ya meza ya na kuviweka katikati ya chumba hicho ambacho mapadre hutumia kubadilishia mavazi na vitu vyenye wakfu huhifadhiwa. Kwaya ya Mtakatifu Joseph iliendelea kuongoza kwa nyimbo mbalimbali kama ile ya ?Nakupenda Maria?, ?Jina Maria? na ?Enendeni Duniani Kote?. Wakati nyimbo hizo zikiendelea kuimbwa, Padre Minja na Vivian walikaa kitako ili kusikiliza maungamo ya Charles Mugisha; maungamo ambayo yalichelewesha ufungaji wa ndoa ya njiwa hao wawili wapendanao. Baada ya sekunde chache kupita na baada ya kuvuta pumzi ndefu, Charles alianza kusimulia ni kitu gani kilimfanya asitishe mwitikio wake wa ndoa. Padre Minja na Vivian kama wanafunzi watulivu darasani, walisikiliza kwa makini.

* * *

Hadi mwaka 1990 nikiwa na miaka 25 nilikuwa bado mimi bikira. Nilikuwa sijawahi kulala na mwanamke zaidi ya kuishia kuwatamani tu kwa nje. Bila ya shaka utajiuliza ilikuwaje nichelewe kiasi hicho kuanza mapenzi. Ukweli wa mambo ni kuwa mimi nilikuwa ni mseminari wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza na mwaka huo ulikuwa ni mwaka wangu wa mwisho kabla sijapandishwa kwenye madaraja ya altare, yaani ushemasi na baadaye Upadre. Moyoni mwangu niliamini kabisa kuwa mimi nilikuwa na wito wa upadre na tangu utoto nilijiandaa kutimiza ndoto hiyo.

Ni kwa sababu hiyo basi niliwakwepa kinadada kama wana ukoma, na kila nikimuona dada mwenye kuvutia nilijikuta nikisali sala ya baba yetu nikirudia rudia maneno ya ?usitutie majaribuni? mara nyingi. Niliweza kutawala tamaa zangu hasa kwa kupenda kujisomea vitabu mbalimbali vya kitaaluma, kuandika, na kufanya kazi nyingi za mikono. Muda wangu mwingi wa ziada nilikuwa natembelea wagonjwa, kushiriki katika kwaya, na kufundisha tuition vijana wa sekondari hasa masomo ya Fizikia na Kemia. Niliyapenda maisha yangu na sikuwa na shaka kabisa kuwa nitakuwa padre mzuri, mcha Mungu, na mtumishi wa watu.

Ndoto yangu hiyo ilipeperuka siku ile isiyo na jina, miezi mitatu kamili kabila sijavikwa ushemasi kwenye ibada ya Misa Takatifu kwenye viwanja vya jangwani ambayo ilikuwa iongozwe na Baba Mtakatifu Yohanne Paulo II akiwa katika ziara yake ya Kichungaji. Nilikuwa katika mapumziko ya mwisho toka seminari ya Kipalapala, siku ile ambapo mambo yote yaliniharibikia na mwelekeo wa maisha yangu kubadilishwa. Wakati wa mapumziko hayo ya karibu miezi miwili nilikuwa nimefikia parokia ya Pugu ambako nilikuwa nasaidia shughuli mbalimbali pale parokiani. Licha ya kusaidia parokia ya Pugu mara nyingi mida ya mchana nilikuwa nakuja St. Joseph kwa kusaidia kazi mbalimbali za ofisini na kupata uzoefu wa kikazi. Nilikuwa ni mwanafunzi wa Padre Peter Mhonda aliyekuwa msaidizi wa Askofu wa Dar. Niliona fahari kila nikija hapa na kushirikia katika misa, huduma mbalimbali na shughuli mbalimbali.

Siku hiyo hata hivyo nilikuwa nimemaliza shughuli zangu mapema St. Joseph na Sr. Maria Goretti alinichukua kwa gari hadi eneo la Tazara ambako nilikuwa kwa kawaida nasubiri mabasi ya kwenda Pugu. Ilikuwa jioni kwenye majira ya saa kumi na mbili hivi wakati jua limeanza kutua ingawa joto la Dar bado liliendelea nilikuwa nimekaa chini ya Kibanda cha kusubiria mabasi kilichoko nje ya jengo la Tazara ikiangalia upande wa Buguruni. Nilikuwa nimevalia nguo za kawaida tu zilizonifanya nionekane kama mfanyakazi wa kampuni fulani na mkononi nilikuwa nimeshika gazeti la Alasiri ambalo ndio lilikuwa limetinga mitaani mida hiyo.

(Itaendelea kesho)

Kepa
11-27-2008, 12:35 AM
I can't wait to read it kesho!!!

mwanakijiji
11-28-2008, 09:05 AM
(Inaendelea)

Pembeni ya kibanda hicho cha abiria kulikuwa na makontena mawili makubwa ambayo yalikuwa yameunganishwa na kufanya yawe kama jengo dogo. Makontena hayo yalikuwa yanatumiwa na mama mmoja wa kichagga aliyekuwa anaagiza vifaranga vya kuku toka Zambia. Hivyo nje ya makontena hayo kulikuwa na maboksi yenye matundu tundu ambayo yamejazwa vifaranga. Huku nikiendelea kusoma gazeti langu la Alasiri nilikuwa naangalia watu mbalimbali waliokuwa wanapokea vifaranga vyao toka kwa mama huyo na wasaidizi wake. Nikajisemea moyoni kuwa hayo ndiyo maisha kweli.

Nikiwa nimezama kwenye mawazo ya biashara na nikiendelea kushangaa shangaa watu waliokuwa wanapita pita kutoka upande wa Tazara kwenda upande mwingine wa barabara ya Nyerere nilishtushwa na mlio wa kondakta wa daladala aliyekuwa akipiga kelele ?Pugu, Pugu, Pugu!? mara moja nikakunja gazeti langu na kuwa miongoni mwa watu wa tano ambao tulikuwa tunasubiri basi hilo la kwenda Pugu. Nilifanya hima na mimi kukimbilia kwenye mlango wa daladala hilo kwani basi jingine la kwenda huko Pugu lilikuwa linakuja kama kila baaada ya nusu saa hivi. Nikajibanza banza na kujipenyeza penyeza katika msongamano wa watu. Harufu ya jasho, uchafu, na manukato ilichanganyika ndani ya basi hilo huko watu wakiwa wamebanana katikati ya njia ya kupita. Nilijitahidi hadi kufika katikati ya basi ambapo kama wengine nilinyanyua mkono wangu wa kulia na na kushikilia mtalimbo ulioanzia karibu na kiti cha dereva hadi mwisho wa basi. Mkono wangu mwingine nilikuwa nimeshikilia gazeti langu nililokuwa nikililosoma pale kituoni. Upande wa kulia kulikuwa na mtoto aliyekuwa analia utadhani ametumwa kwani alikuwa habembelezeki na hakukuwa na ujanja ili kuzoea kelel hizo za mtoto. Na pande zote nilikuwa nimebanwa na watu waliokuwa wamesimama.

Mara tu baada ya abiria wa mwisho kuingia konda akaanza kulipiga piga basi ubavuni kumuashiria dereva kuwa muda wa kuondoa kituoni umefika, huku akikimbia pembeni yake na kudandia kwa mguu wake wa kusho alipiga kelele ?imetoka hiyo?. Basi likaanza kuchanja mbuga. Huku muziki wa Kanda Bongoman wa ?Inde Monie? ukikoroma kwenye spika kuu kuu za basi hilo, safari ya kurudi Pugu ilianza.

Mtikisiko na kuyumba yumba kwa basi likiyapita magari mengine kwenye barabara hiyo mashuhuru ya Nyerere (zamani ikijulikana kama Pugu) ulinifanya nigundue kuwa Uanaume wangu umeanza kuamka kutoka katika mapango ya madongo kuinama. Kisa na mkasa ilikuwa ni dada aliyekuwa naye amesimama mbele yangu na makalio yake yakiwa karibu kabisa na eneo langu ?nyeti?. Mara moja nilianza kujisikia vibaya na kuwa na hisia ya hatia. Nilijihisa kama ?mbakaji? kwani kwa kijana mseminari kama mimi kuanza kumwakia tamaa ndani ya basi ilikuwa ni kama nafanya dhambi ya mauti. Hata hivyo sikuwa na ujanja, niliporudi nyuma, basi lilipunguza mwengo na kujikuta nasukumwa mbele na ?kugongana? na matako ya mviringo kama wa kitunguu ya dada yule. Cha kushangaza ni kuwa yeye mwenyewe alikuwa kama hasikii, yaani ilikuwa kama nagongana na sponji.

Kijasho chembachemba kilianza kunitoka usoni na kingine kilianza kutiririka kwenye kwapa ya mkono wangu ulioinuliwa juu na niliweza kukihishi kikiteremka taratibu upande wa kulia wa mbavu zangu. Yule dada aliyekuwa mbele yangu aligeuza shingo yake kuniangalia. Nilihisi nimebambwa. Macho yetu yalipogongana alitabasamu na kucheka kidogo. Badala kusogea mbele, akajirudisha nyuma zaidi na hapo nikagundua kuwa nimepatwa na mfadhaiko. Nilihisi kigugumizi kimenishika na kiu kikinikaba. Kwa kadiri gari lilivyokuwa linabadilisha mwenzo na kunesa nesa ndiyo dada yule alivyoanza naye kutingisha kiuno chake taratibu akikisugua mbele ya suruali yangu. Alikuwa anafanya kama mchezaji wa ile ngoma ya kimakonde ya Sindimba, isipokuwa alikuwa anafanya kwa ?slow motion?. Hisia zikanizidia na kama mtu ambaye nimepagawa nikajikuta ?nimefika? papo kwa papo. Mwili ulihisi raha ajabu, lakini roho yangu ilihisi uchafu na dhambi kubwa. Nilitamani, ardhi ipasuke na kunimeza, lakini wakati huo huo nikitimani yule dada afanye tena kabla ya hiyo ardhi kupasuka!


Sura ya II

?Baba padre, nawahadithia kisa hiki si kwa sababu nataka kujisifia ila kuwaonesha nilikotoka ni wapi na nitakapotoa uamuzi wangu ujue nimeutoa nikiwa na mawazo yapi.? Mugisha alisema huku akimeza fundo kubwa la mate.

Padre Minja alihisi joto likianza kumpanda kwa ghafla. Ikabidi alegeze tai yake ya kiromani. Bibi harusi alikuwa amebakia mdomo wazi, hakujua akimbie, alie, acheke au afanye nini.

* * *

Giza lilikuwa limeanza kuingia na abiria wengi walianza kuteremka kwenye vituo mbalimbali na wengi walishuka maeneo ya Gongo la Mboto, Ukonga, na Kipunguni. Baada ya kupita Kipunguni basi lilikuwa na watu walioketi kwenye viti na mimi nikapata nafasi kwenye kiti cha nyuma kabisa. Niliamua kujibanza upande wa kushoto wa kiti karibu na dirisha. Upande wa kulia kulikuwa na mtu mmoja ambaye sikuweza kumtambua kutokana na giza kama alikuwa ni kijana, mtu wa makamu au mzee. Ila najua alikuwa kimya tu. Yule dada naye akaja kukaa kwenye kiti kile cha mwisho na kujisogeza upande wangu. Nilihisi miguu yangu inatetemeka na moyo wangu karibu unitokee mdomoni.

?Usiogope mimi siyo jinni? alisema kwa sauti ya upole, iliyoyajaa aibu lakini ikionesha kujiamini.

?Na kama wewe ni jinni basi ushindwe na kulegea!? Nilisema huku nikimung?unya mung?unya maneno.

Dada akaanguka kicheko cha dharau.

?Mbona unakuwa kama hujawahi kufanya mapenzi? aliniuliza huku akiwea mkono wake kwenye mapaja yangu. Nilihisi ashki ikipanda mwilini kama umeme kuanzia utosini hadi kwenye nyayo.

?Duh! Mbona unanisoma kama nimeandikwa kwenye paji la uso? nilijimudu kusema. Nikaamua kumwambia ukweli, kuwa mimi nilikuwa ni mseminari na haturuhusiwi kufanya mapenzi. Huyo dada aliyejitambulisha kwa jina la Blandy aliangusha kicheko cha mwaka.

?Yaani hujawahi kufanya kabisa?? aliuliza kwa udadisi huko macho yake kayakodoa kuniangalia.

?Kabisa? nilimjibu kwa ufupi huku nikiangalia dirishani.

?leo siku yako ya bahati, frateri? alisema. Kabla sijageuka kumwangalia, mkono wake uliokuwa kwenye mapaja yangu ulianza kufungua mkanda wa suruali yangu. Nilitamani nimkataze lakini nilikuwa kama nimepigwa ganzi. Nikafikiri haraka haraka ?mara moja tu? si vibaya. Mafundisho yote ya dini niliyopewa yalianza kupeperuka kama vumbi. Nilikuwa kama ?ndege mjanja?! Nilinaswa nikanasika. Nikiwa bado nashangaa shangaa, Blandy alianza kunifanyia mambo ambayo nilikuwa nayasikia tu vijiweni. Alianza kunitafutana utadhani asiponitafuna atahukumiwa kifo.

Niliishiwa nguvu na mwili wangu ulikuwa unatetemeka kwa raha. Akili yangu iliniambia ?hapana? lakini mwili wangu ulikuwa unapiga kelele ya ?ndiyo ndiyo?. Blandy alikuwa ni fundi wa hicho alichokuwa anafanya na sijui alijuaje maana nilipokaribia kufika mwisho akaacha. Nusura nimshikilie kichwa hadi amalize. Lakini hakuwa amefikia mwisho. Huku zikiwa zimebaki kama dakika kumi hivi hadi kufika Pugu, Blandy aliamua kunikalia huku mikono yake ikiwa imeshikilia kiti kilichokuwa mbele yetu. Alichofanya hapo sitaweza kusahau, kwani siku hiyo nilitolewa ushamba na kuingizwa mjini. Blandy alikuwa ni msichana wangu wa kwanza.

Tulipofika mwisho wa kituo tuliagana huku nikiwa nimechanganyikiwa. Sikujua kama nimbembeleze nimuone tena au ndio niache vilivyokwenda kwa mganga. Yeye hakusema maneno mengi, ila aliniambia ?Ukiwa padre utakuwa na njaa sana?. Sikuelewa maana yake kwani niliporudi nyumba ya mapadre (rectori) walikuwa wamenibakishia chakula huku nyumba nzima ikiwa kwenye kikanisa kidogo kwa sala za jioni. Sikuweza kula, nilienda moja kwa moja chumbani na kujifungia. Haikunichukua muda, nikapitiwa na usingizi mnono, usingizi fofo, usingizi kama wa pono.

Kesho yake nilipoamka nilijisikia unyonge wa roho. Nilitamani nifanye ?maungamo?. Hata nilijua kuwa sikuwa tayari kufanya maungamo mazuri kwani mawazo yangu yote nilikuwa namuwaza Blandy. Nilihisi roho yangu inaninyong?onyea kwa kumuwaza dada yule. Hata hivyo sikuwa na muda mrefu sana kwani safari yangu ya kwenda Mwanza kuwaona wazazi na askofu Mkuu Mayala ilikuwa tayari na siku ya Alhamisi majira ya saa kumi na moja nilipanda treni kuelekewa Mji huo ulioko kando ya Ziwa Victoria.

(Itaendelea kesho)

My more
12-12-2008, 10:44 AM
Kesho ya Makange?:D:D

FirstLady
04-08-2010, 01:29 PM
mbona haiendelei mpaka miaka miwili imepita?