mwanakijiji
11-26-2008, 05:19 PM
Kuna kila dalili kuwa wingu la kuwajibishana limeanza kumzunguka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Dr. Edward Hosea. Vyanzo vyetu vya uhakika vimemnong'oneza "nzi" wetu anayeruka ruka kila kukicha kuwa yale mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dr. Harrison Mwakyembe (CCM, Kyela) yako karibu kutimilika kwenye suala la Dr. Hosea.
Ripoti ya Dr. Mwakyembe iltaka idara na watumishi mbalimbali wa serikali kuwajibishwa, miongoni mwao ni TAKUKURU ambayo Kamati Teule ilisema kuwa haikufanya kazi yake vizuri hasa baada ya Dr. Hosea kutokea hadharani na kutetea mkataba wa Richmond na h ivyo "kuisafisha" kampuni hiyo.
Ni katika minajili hiyo, habari zilizoanza kuingia siku chache zilizopita zinaelekeza katika kumuwajibisha Dr. Hosea aidha kwa kumsimamisha kazi kwa muda (kitu ambacho kuna watu wanaona ni bora zaidi) na kumuondoa TAKUKURU.
"Kumuondoa laweza kuwa ni jambo gumu kidogo kwa wakati huu" amedokeza mtonyaji wetu. Sababu kubwa ni kuwa "timing" yao itakuwa mbaya hasa baada ya TAKUKURU kuleta kesi dhidi ya waliowahi kuwa Mawaziri wenye nguvu sana kiasi kwamba kumuondoa Hosea siku chache baadaye itakuwa ni kama kulipiza kisasi.
"Wapo wanaoogopa kumgeuza Dr. Hosea kuwa ni John Githongo wa Kenya na kumfanya awe shujaa". Anasema mtonyaji wetu.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ni kuhakikisha kuwa kwa namna fulani Dr. Hosea anawajibika na kuadhibiwa wakati huo huo kutokumuadhibu kiasi cha kumfanya awe "mbogo" na kujitetea kuwa "anaonewa kwa sababu ameanza kufanya kazi yake kweli na kuwashtaki vigogo".
Wakati huo huo, watumishi wengine waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati Teule wataanza kuchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu wakati wowote kuanzia sasa na kabla ya mwaka mpya lengo likiwa mapendekezo yote ya Kamati yawe yamekamilishwa ifikapo kikao kijacho cha Bunge la Januari.
Tovuti yako, inafuatilia jambo hili kwa makini.