PDA

View Full Version : Ya kuchoma vibaka! adhabu na kosa (Picha 18+)

mwanakijiji
11-26-2008, 07:08 PM
Hivi kweli adhabu ya kuchomolewa ni kifo? Hawa watu wenye ujasiri wa kutia watu wengine "kiberiti" kwa makosa ya usumbufu na kero kwanini na wenyewe wasitiwe pingu? Kama wale waliopopoa msafara wa Rais waliweza kutafutwa kwa udi na uvumba, ni mpaka lini vitendo hivi vya kinyama na vilivyozoelewa vitakomeshwa?

Kweli sisi bado tuna tabia za kijima namna hii?

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1227681970_kibaka.jpg

http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1227681970_kibaka_1.jpg

kweli tutafika na mawazo ya namna hii?

Kepa
11-26-2008, 08:10 PM
Ambaye hajawahi kuiba hata siku moja au kusababisha wizi uwe wa majibu katika chumba cha mtihani, uwe wa mke mume wa watu, uwe wa pesa, au ule wa kutotoa sadaka kwa Mungu awe wa kwanza kupiga jiwe la kwanza!!!

Awe wa kwanza kutoa hukumu- kwa lugha rahisi

mwanakijiji
11-26-2008, 10:16 PM
Ambaye hajawahi kuiba hata siku moja au kusababisha wizi uwe wa majibu katika chumba cha mtihani, uwe wa mke mume wa watu, uwe wa pesa, au ule wa kutotoa sadaka kwa Mungu awe wa kwanza kupiga jiwe la kwanza!!!

Awe wa kwanza kutoa hukumu- kwa lugha rahisi

Mimi binafsi kwa kweli ningependa kumuona huyo mtu wa kwanza kuweka kuni juu ya mwanadamu mwenzie namna hiyo.. ! Nafikiri ni hisia watu wanafikiri wana nguvu juu ya uhai wa mtu mwingine..