View Full Version : Kipanya mchokozi...
mwanakijiji
11-26-2008, 07:17 PM
Kipanya kaja na katuni hii:..
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/gallery/mkapahandaki.jpg
ambayo ikanikumbusha kisa cha Rais mwingine..
http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/c/c6/SaddamSpiderHole.jpg
Maono hayo Mzee wangu...!!
Mmmm inakoelekea kama vile imekaribia.....itakafika hapo rangi ya katiba itabidi iwe dark tan
kuonyesha ukomavu wa mwafrika (mtanzania) katika siasa.
anonymous
11-27-2008, 03:46 AM
ah!!! Mimi sioni lolote litakalotokea. Kwani Mkapa mwenyewe hajajificha kokote kule. Na ana ulinzi wa kueleweka kuliko sisi wadanganyika wenyewe. Piga ua, hakuna cha andaki wala kaburi.
Si wadanganyika wenyewe tusipomchimbia huko chini je unafikiria Mafisadi kama akina Kikwete eti ndio watamchimbia. PIGA UA GARAGAZA. Ataendelea kupeta tu mpaka tupate akili timamu.
mwanakijiji
11-27-2008, 07:53 AM
Anon.. usikate tamaa bado kuna njia moja ya kumwajibisha.. subiri mwakani utaona.. nguvu ya kutawala inatoka kwa watu na inabakia kwa watu!
Mpita Njia
11-27-2008, 10:24 AM
Anon.. usikate tamaa bado kuna njia moja ya kumwajibisha.. subiri mwakani utaona.. nguvu ya kutawala inatoka kwa watu na inabakia kwa watu!
Nadhani hapo ndipo nchi itakapotikisika kama tulivyotishiwa!!!
mwanakijiji
11-27-2008, 10:35 AM
Nitajaribu kuchambua kinachoendelea sasa hivi ili kukiweka katika mwanga unaostahili. Nadhani watu wasiruke ruke kwa furaha lakivi vile vile wasife moyo.
anonymous
11-27-2008, 11:53 AM
Anon.. usikate tamaa bado kuna njia moja ya kumwajibisha.. subiri mwakani utaona.. nguvu ya kutawala inatoka kwa watu na inabakia kwa watu!
Tumelelewa katika nchi ya mazingaombwe kiasi kwamba hata waigizaji wenyewe wanataka kutushawishi kuwa eti ni tuu ndani ya Ulimwengu wa kweli ili hali wao wanajua kabisa watutendacho.
Hivi ndivyo tulivyolelewa.
Na nakuambia Mzee Mwanakijiji kuwa hata hii ni sehemu fulani tu ya maigizo na naona wengi wanatumai na kuona mwisho ukifika basi tutaachana na GIZA hili lakini ukweli unabaki pale pale kuwa waigizaji wanaipenda kazi yao na SHOW bado inaendelea.
Hii inawezakuwa tu sehemu uliyoipenda ya MAIGIZO lakini kumbuka SHOW INAENDELEA Mzee Mwanakijiji.
Mpita Njia
11-27-2008, 01:18 PM
Nitajaribu kuchambua kinachoendelea sasa hivi ili kukiweka katika mwanga unaostahili. Nadhani watu wasiruke ruke kwa furaha lakivi vile vile wasife moyo.
Mh! Huu utani mwingine huu!!! lol
My more
11-30-2008, 02:59 AM
Anon.. usikate tamaa bado kuna njia moja ya kumwajibisha.. subiri mwakani utaona.. nguvu ya kutawala inatoka kwa watu na inabakia kwa watu!
Kusubiri tena?
magoma
12-02-2008, 07:36 PM
Kusubiri tena?
Lisemwalo lipo kama halipo laja!!!(tukumbuke methali za mababu zetu) na mbio za sakafuni huishia ukingoni!! huyu bwana BWM aliwahi kutwambia watanzania tuna wivu wa kijinga na atawalinda wawekezaji kwa nguvu zake zote kumbe naye alikuwa investor pale KIWIRA akiwa rais wa nchi, katiba ya nchi haisemi hivyo. iko cku atanyea ndoo tu pale segerea/keko/ukonga kama rafiki zake bwana yona na mramba walivyonyea ndo kwa week nzima pale keko.
Mungu tusaidie sisi wanao, nadhani baba wa taifa(JK Nyerere) huko uliko unayaona haya yanayotokea hapa Bongoland.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.